July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wabunge, waandishi wamlilia Kamukara

Marehemu Edson Kamukara enzi za uhai wake

Spread the love

WAANDISHI pamoja na wabunge kwa ujumla wao wamesikitihwa na kifo cha mwandishi wa habari Edson Kamukara kilichotokea jana nyumbani kwake Mabibo jijini Dar Es Salaam.

Wabunge wameonesha hisia zao juu ya kifo cha mwandishi huyo ni mbunge wa Kisarawe, Suleimani Jafo (CCM), Felix Mkosamali (NCCR Mageuzi), Prof. Kulikoyela Kahigi (Chadema), Conchester Rwamlaza (Chadema), David Kafulila (NCCR-Mageuzi) ambao kwa pamoja wamesema kuwa kifo hicho ni pengo kubwa kwa tasnia ya habari.

Kwa upande wa waandishi wa habari kwa ujumla ni waandishi wote wa habari za bunge, pamoja na waandishi waliopo nje ya bunge akiwepo Hamida Ramadhani(Tanzania Daima), Ramadhani Hasani (Mtanzania), Stanslaus Likomawage (Radio mwangaza), Sharifa Mdeme (Raia Tanzania) na Nazael Mkiramweni (Gazeti la Majira).

Wakizungumzia kifo cha mwandishi huyo walisema ni pigo kubwa na kuna kila sababu ya kufanya uchunguzi wa kina juu ya kifo chake.

“Namjua Kamukara alivyokuwa akifanya kazi zake katika kiwangi sitaki kusema lolote juu ya kifo chake lakini ni vyema kwa sasa wale wote wenye mlengo wa kimageuzi mkafanya kazi kwa taadhari kubwa,” amesema Prof. Kahigi.

Naye Mbunge wa Kisarawe Suleimani Jafo, amesema kifo  cha Kamukara kimewashtua watu wengi kwani kifo chake ni pigo kubwa kwa tasnia ya habari jambo ambalo ni hatari zaidi.

“Kimsingi mimi nimeumia sana kwani kuna program moja ya kazi nilikuwa nikisubiri muda wa saa sita ufike ili niweze kumpigia simu tuweze kuwasiliana naye lakini nilipata taabu sana kuamini pale nilipopata ujumbe mfupi kuwa amefariki.

“Jambo hili linatia simanzi lakini tumuombe Mungu atupe wepesi na napenda kuwapa pole wanahabari wote kwa ujumla mliopo hapa bungeni na wale ambao wapo nje ya bunge.

“Zaidi Mungu awajarie uvumilivu wanafamilia najua jambo hili ni zito lakini lakini hakuna jinsi ni Mungu pekee anayeweza kutetea,” amesema Jafo.

error: Content is protected !!