Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wabunge waanza kubaguana waziwazi
Habari za Siasa

Wabunge waanza kubaguana waziwazi

Jesca Kishoa, Mbunge wa Viti Maalum Chadema
Spread the love

MBUNGE wa Viti Maalum Jesca Kishoa (Chadema) ameibana serikali na kuitaka itangaze kama wabunge wa Viti Maalum bila kujali vyama vyao waondoe bendera za bunge na badala yake waweke bendera za vyama vyao, anaandika Dany Tibason.

Kishoa alitoa hoja hiyo bungeni alipokuwa akiomba mwongozo wa spika juu ya kutofautiana kwa kauli za viongozi kutokana na ubaguzi kati ya wabunge wa Viti Maalum na wabunge wa majimbo.

Akiomba mwongozo wa Spika Kishoa amesema kuwa ni jambo baya kuwepo kwa ubaguzi kwa wabunge bila kujali itikadi za vyama vya siasa.

“Mheshimiwa Spika mimi naomba mwongozo wako, unajua hakuna jambo baya la ubaguzi katika bunge kwa kuwabagua wabunge wa majimbo na wabunge wa Viti Maalum ili naliongea bila kujali itikadi za vyama.

“Ndiyo maana wabunge wote tunapata mishahara sawa lakini hivi karibuni ilitangazwa wabunge wa majimbo kufanya mikutano katika maeneo yao pamoja na wabunge wa Mikoa ambao ni wabunge wa viti maalum

“Lakini kwa kauli ya Waziri Mkuu ametangaza kuwa wabunge wa Viti maalum hawana uwezo wa kufanya mikutano sasa nataka mwongozo wa Spika kama wabunge wa viti maalum hawatambuliwi ni kwanini tusiruhusiwe kuondoa bendera za bunge ili tuweke bendera za vyama vyetu ili tufanye mikutano katika mikoa yetu,” alihoji Kishoa.

Hata hivyo Spika aliingilia kati mwongozo wa Kishoa huku akisema kuwa hakuna mbunge hata mmoja wa viti maalum ambaye ni mbunge wa mkoa bali wamejiwekea utaratibu wenyewe.

Aidha amesema kuwa uenda wabunge hawakumuelewa vizuri waziri mkuu kwani alisema kuwa kila mbunge atafanya mikutano na watu ambao walimchagua kuwa mbunge.

“Uenda wabunge hamkumuelewa vyema Waziri Mkuu lakini alichosema ni kuwa kila mbunge atafanya mikutano na watu wake waliomchagua, Je nyie mlichaguliwa na akina nani na mkoa mzima.

“Hata hapa hawa niliowaapisha wametoka mikoa gani hapa labda tufanye kitu kimoja mimi na Waziri Mkuu pamoja na katibu wa bunge tuweze kukaa pamoja ili kutoa elimu kwenu mfano mzuri hapa kuna Naibu wa Spika je yeye anatoka mkoa gani?” alihoji Spika.

Hata hivyo wabunge wengi wa viti maalum hususani wanaotoka vyama vya upinzani wamedai kuwa kwa sasa wananyimwa fursa ya kufanya siasa jambo ambalo walisema ni kutokutendewa haki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

error: Content is protected !!