September 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wabunge wa Simba na Yanga vitani

Spread the love

WABUNGE wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambao ni mashabiki wa klabu za Simba na Yanga, wanatarajia kucheza mchezo maalum wa mpira wa miguu wenye lengo la kukusanya fedha zitakazosaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera, anaandika Aisha Amran.

Mchezo huo utakaochezwa siku ya Jumapili ya wiki hii, tarehe 25 Septemba katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam unatarajia kuvutia mashabiki wengi hasa kutokana na hali ya kisiasa iliyopo nchini kwa sasa.

William Ngeleja, Mwenyekiti wa timu hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Sengerema, mkoani Mwanza amewaomba watanzania na mashirika mbalimbali kuchangia kwa kununua tiketi za mchezo huo ili kupatikana kwa fedha ambazo zitapelekwa kwa wahanga wa tukio hilo.

Kingilio cha chini katika mchezo huo kitakuwa shilingi 3,000/- kwa viti vya bluu na kijani,  Shilingi 10,000/- na 15,000/- kwa viti vya rangi ya Machungwa huku katika viti vya watu maalumu (VIP) kiingilio kikitarajiwa kuwa shilingi 50,000/-, 100,000/- na 200,000/-.

Hata hivyo, jumla ya tiketi 50 katika eneo la viti vya sehemu ya watu maalumu zitauzwa kwa shilingi 1,000,000/-

Mechi hiyo itatanguliwa na mchezo wa utangulizi baina ya timu ya wasanii wa filamu maarufu kama ‘Bongo Movie’ dhidi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva).

error: Content is protected !!