January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wabunge wa CUF kutinga mahakamani

Mbunge wa Mkanyageni, Mohammed Habib Mnyaa

Spread the love

WABUNGE wa Chama cha Wananchi (CUF), wametangaza kuwaburuza mahakamani Ofisa mdhamini wa Vitambusho vya Taifa vya Mzanzibari (ZAN-ID) Pemba, Hamadi Selemani na Ofisa vitambulisho Wilaya ya Mkoani, Omar Ngwali. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Wamesema kuwa kusudio la kuwaburuza mahakamani maofisa hao ni kutokana na kuzuia haki ya kutowapa vitambulisho vya makazi watu 422, jambo ambalo linapelekea kushindwa kujiandikisha katika daftari la Tume ya Taifa Zanzibar (ZEC).

Kwa niaba ya wabunge na wawakilishi hao, Mbunge wa Mkanyageni, Mohammed Habib Mnyaa, amesema walalamikiwa hao wameshindwa kuwaandikisha wananchi hao katika daftari huku wakiendelea kuwanyima vitambulisho vyao vya ZEC.

Mnyaa amesema “kutokana na kauli ya mkuu wa wilaya, nawataka wabunge pamoja na wawakilishi kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa ajili ya kujiandikisha katika daftari la kupiga kura.”

Amesema kutokana na kauli hiyo ya mkuu wa wilaya, viongozi wengi pamoja na wabunge na wawakilishi waliamini kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kafanya hivyo.

“Sisi wabunge na wawakilishi tuliwahamasisha wananchi kwenda mkoani kwa wingi kuchukua vitambulisho kwa wale waliopiga picha na kuomba vitambulisho hivyo pamoja na wale ambao vitambulisho vyao vya zamamani vimekwisha muda kupaswa kuchukua vipya,”amesema.

Kwa kujibu wa kauli ya mkuu wa wilaya katika kikao hicho, palikuwepo na vitambulisho zaidi ya elfu nne ambavyo havijachukuliwa na wenyewe.

Mnyaa ameongeza kuwa, wabunge pamoja na wawakilishi wakiwa wamefuatana na wananchi katika majimbo ambayo mara kadhaa walikuwa wakienda mkoani –ofisi ya vitambulisho kwa kuchukua vitambulisho vyao, lakini kwa makusudi walinyimwa na kuambiwa bado havijafika.

Amesema kuwa wakati mwingine wananchi walikuwa wakiambiwa kuwa uzalishaji wa vitatambulisho hivyo umesimama kwa sababu ofisi ya vitambulisho Zanzibar hawakuingiziwa fedha kwa mujibu wa bajeti yao waliyoomba na mara nyingine sababu ya vifaa vya kuzalisha vitambulisho vimekwisha.

“Haya yote yakitokea kwa upande wa wanachama wa CCM wao hakuna shida malalamiko yoyote na wakipiga picha baada ya wiki mbili wanapatiwa vitambulisho vyao hata walio chini ya umri wa miaka 18,” amesema Mnyaa.

error: Content is protected !!