Sunday , 29 January 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Wabunge Uganda washtakiwa kwa ugaidi
Kimataifa

Wabunge Uganda washtakiwa kwa ugaidi

Bobi Wine (kushoto) na Allan Ssewanyana
Spread the love

 

WAENDESHA mashtaka nchini Uganda wamewaongezea mashtaka ya ugaidi wabunge wawili wa chama cha upinzani nchini humo – National Unity Party (NUP). Anaripoti Glorry Massamu TUDARCo … (endelea).

Wabunge hao – Mohammed Ssegirinya na Allan Ssewanyana ambao ni washirika wa kiongozi wa upinzani, Bobi Wine – walikuwa meshtakiwa kwa makosa matatu ya mauaji na shitaka moja la kujaribu kuua linalohusiana na mauaji yaliyotokea katika eneo la kati la Uganda la Masaka.

Wabunge hao walifikishwa mbele ya Hakimu mkazi wa Masaka kwa njia ya video kutoka katika gerezani katika wilaya ya Wakiso.

Muhammed Ssegirinya

Wabunge hao hawakujibu lolote kuhusiana na mashitaka hayo ikiwamo hilo la kula njama kutaka kufanya ugaidi.

Jumla ya watu 23 hadi sasa wameshtakiwa kwa mauaji ambayo watekelezaji wake wanawalenga kwa mapanga wazee wanaoendelea na kazi nyumbani au wanaofanya kazi usiku.

Kikosi cha pamoja cha maofisa wa usalama kwa sasa kinafanya uchunguzi katika eneo hilo.

Mashambulio ya aina hiyo yalitokea katika eneo hilo hilo katika miaka ya 2009, 2017 na 2018.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

DCI ajitosa uchunguzi matokeo uchaguzi mkuu Kenya

Spread the loveOFISI ya Mkurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI)...

HabariKimataifa

Aliyesomeshwa na mchumba aamuriwa kurudisha Sh 9.4 Mil. baada ya kukataa kuolewa

Spread the love  MWANAMKE mmoja nchini Uganda ambaye aliuumiza moyo wa mchumba...

Kimataifa

Uganda yaanza kuchimba mafuta

Spread the love  UCHIMBAJI wa kwanza wa mafuta kibiashara nchini Uganda umeanza...

Kimataifa

Afrika kusini waandamana kushinikiza serikali kumaliza tatizo la umeme

Spread the love  MAMIA ya wafuasi wa Chama cha upinzani nchini Afrika...

error: Content is protected !!