January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wabunge: Tozo ya mafuta itaharibu misitu

Moja ya misitu iliyopo nchini Tanzania

Spread the love

WAKATI Serikali ikipandisha tozo katika nishati ya mafuta, wabunge wameonyesha wasiwasi kuwa misitu itaharibiwa zaidi, hivyo jitihada zaidi zinahitajika kuilinda. Anaandika  Jimmy Mfuru, Dodoma … (endelea).

Badala yake, wabunge wametakiwa kuishauri serikali kuongeza bajeti katika suala la kuhifadhi misitu kwa kuendeleza jitihada zinazofanywa na mradi wa mkaa endelevu unaofanyika katika vijiji vya Kilosa mkoani Morogoro.

Mkutano huo ulioshirikisha Kamati mbili za Bunge za Ardhi, Maliasili na Mazingira na Nishati na Madini ulifanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.

“Inatakiwa sisi wabunge pamoja na wanasiasa wengine kuendelea kuunga mkono mradi huu wa mkaa endelevu unaoendeshwa na shirika hili kupanda kwa tozo katika mafuta kutapelekea misitu kuharibiwa zaidi, hivyo jitihada zinahitajika kuilinda”, amesema Suzan Kiwanga wa Viti Maalum (Chadema).

Serikali imetangaza tozo mpya ya Sh.100 kwa mafuta ya dizeli kutoka Sh. 50 kwa lita, huku mafuta ya taa yakiongezwa tozo kufikia Sh.150 kutoka Sh.50. Hoja ya serikali ni kudhibiti uchakachuaji wa mafuta.

Kiwanga ametoa kauli hiyo wakati akichangia katika mkutano ulioandaliwa na Shirika la Kuhifadhi Misitu Asilia Tanzania (TFCG) na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) kwa wabunge uliokuwa na lengo la kuwajengea uwezo wabunge juu ya mkaa endelevu.

Hivyo, Kiwanga ameitaka serikali kusaidi jitihada zinazofanywa na shirika hilo ili kulinda misitu kwa kukata miti kwa ajili ya mkaa kitaalamu kuliko kukata kiholela na kufanya uharibifu wa mazingira.

Naye, mbunge wa Viti Maalum (CCM), Martha Mlata, amewataka wabunge kupigania fedha ziongezwe katika bajeti ili kulinda misitu kwa kuwa ni nishati ambayo inatumiwa na Watanzania wengi na kuwataka wagombea wa nafasi mbalimbali kuelimisha wananchi juu ya uchomaji wa mkaa endelevu.

error: Content is protected !!