October 23, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wabunge CCM wapitisha mswada kibabe

Spika wa Bunge, Anna Makinda

Spread the love

BUNGE limepitisha Mswada wa sheria ya usimamizi wa mafuta na gesi ambao ulikuwa ukijadiliwa  ambao ulisababisha Spika Anna Makinda kuwatimua wabunge 46 wa upinzani. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Mswada huo ambao umepitishwa na wabunge wa CCM licha ya kuwa wachache, pamoja na mbunge wa  Wawi  maarufu kwa jina la mbunge wa mahakama ,Hamadi Rashid Mohammadi (CUF) .

Mbali na kupitishwa mswada huo Manaibu Mawaziri wa Fedha Mwigulu Nchemba na Adam Malima,wametumia muda mwingi kuwashambulia wabunge wa upinzani kwa kitendo chao cha kuondoka bungeni wakati ikiendelea  kujadiliwa bungeni.

Aliyeanza kuwashambulia wabunge wa upinzani ni Mwigulu Nchemba ambaye amlitumia muda mwingi kuwashambulia wabunge hao kwa madai kuwa wanakwamamisha maendeleo kwa kutokubali kupitisha miswada ya mafuta na gesi.

Mbali na hilo alitumia muda mwingi kujinadi kwa maelezo kwamba anasubiria kupitishwa kwa jina lake la kuwania urais ili aweze kutekeleza sheria mbalimbali ambazo zinapitishwa na bunge.

Amesema mambo ya ajabu kuona baadhi ya wabunge wakiendelea kupinga upitishwaji wa miswada kwa kutaka ipitishwe katika bunge lijalo.

Kwa upande wake Malima amesema  hakuna sababu yoyote ya wabunge kupinga miswada ambayo wabunge wa upinzani wameipinga .

Malima kama ilivyokuwa kwa Mwigulu nae alitumia muda mwingi kuwabeza na kuwadharau wapinzania ambao walikataa kupitisha mswada huo.

error: Content is protected !!