Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wabunge CCM wachuana kumrithi Dk. Tulia
Habari za SiasaTangulizi

Wabunge CCM wachuana kumrithi Dk. Tulia

Abdullah Ally Mwinyi
Spread the love

 

WABUNGE wa chama tawala nchini Tanzania- Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameanza kujitosa kuchukua fomu kuomba kuteuliwa na chama hicho kugombea nafasi ya naibu spika wa Bunge la Taifa hilo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

CCM imefungua dirisha la uchukuaji na urejeshaji fomu za kuwania nafasi hiyo kuanzia jana Ijumaa tarehe 4-6 Februari 2022 ili kujanaza nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Dk. Tulia Ackson.

Dk. Tulia alijiuzulu unaibu spika tarehe 31 Januari 2022, baada ya CCM kumpitisha kuwa mgombea uspika wa Bunge ambapo 1 Februari 2022, alichaguliwa kwa kura zote zilizopigwa na wabunge.

Dk. Tulia alichaguliwa kuchukua nafasi ya Job Ndugai ambaye tarehe 6 Januari 2022, alitangaza kujiuzulu baada ya kukosoa utaratibu wa serikali kuendelea kukopa fedha za kugharamikia miradi ya maendeleo.

Kauli hiyo iliwaibua viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na wale wa Chama Cha Mapinduzi ambao walimshinikiza ajiuzulu naye akafanya hivyo.

Leo Jumamosi, tarehe 5 Februari 2022, Makao Makuu ya CCM ‘White House’ jijini Dodoma, wabunge wa chama hicho wamejitosa kuchukua fomu kuwania kuteuliwa ili kugombea nafasi hiyo katika uchaguzi utakaofanyika 11 Februari 2022.

Mussa Zungu

Baadhi ya waliochukua fomu na majimbo yao kwenye mabano ni, Dk. Hamis Kigwangalla (Nzega Vijijini), Mussa Zungu (Ilala), Abdullah Ally Mwinyi (Mahonda Kaskazini), Mhandisi Samwel Hhayuma Xaday (Hanang’) na David Kiyenzele wa Mufindi Kusini.

Abdullah ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu Ally Hassan Mwinyi amesema amefikia uamuzi huo kwa kuwa ameona ana uzoefu wa kuongoza na hivyo kuamua kuchukua fomu.

“Nina furaha ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa na chama changu nafasi ya Uspika kwani nina uzoefu kwenye masuala ya uongozi,” amesema Abdullah aliyewahi kuwa mbunge wa Afrika Mashariki

Dk. Hamisi Kigwangallah

Sifa nyingine za Abdullah ambaye kitaalamu ni mwanasheria anapewa nafasi kubwa ya kushinda nafasi hiyo hasa ikizingatiwa anatokea Zanzibar ili kudumisha muungano kuwa na viongozi wa muhimili wa Bunge wanaotoka pande zote.

Kwa upande wake, aliyewahi kuwa waziri wa maliasili na utalii, Dk. Kigwangalla amesema amejitokeza kuchukua fomu kutokana na kujiona ana uwezo na sifa za kugombea nafasi hiyo na kwamba chama ndio chenye maamuzi.

Naye Xaday ameeleza ana nia ya dhati na Watanzania hivyo kuamua kuchukua fomu ya kuwania kiti hicho kwa kuwa nafasi hiyo ipo wazi na sifa ya kuwania kiti hicho anayo.

Zungu ambaye ni Mwenyekiti wa Bunge pamoja na Kiyenzele wa wameeleza nia ya kupata nafasi hiyo kwa kuwa uwezo wanao na nia pia wanayo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

error: Content is protected !!