Thursday , 18 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Wabunge 2 mbaroni kwa kupiga mawe helkopta ya Odinga
Kimataifa

Wabunge 2 mbaroni kwa kupiga mawe helkopta ya Odinga

Spread the love

 

WABUNGE wawili kutoka nchini Kenya wanatarajiwa kuhojiwa na Ofisi ya Mlelezi wa Makosa ya Jinai kutokana na tuhuma za kuipiga mawe helkopta ya Mgombea urais nchini humo kutoka ODM, Raila Odinga. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kenya … (endelea).

Wabunge hao Caleb Kositany kutoka Soy na mwenzake wa Kapseret, Oscar Sudi wameeleza kukubali wito wa polisi na kujiwasilisha kwa Ofisi za DCI za Nakuru nchini humo kwa ajili ya kuhojiwa leo tarehe 3 Aprili, 2022.

Aidha, imeelezwa kuwa Spika wa Kaunti ya Uasin Gishu, David Kiplagat naye alikuwa katika afisi za DCI leo asubuhi kuhojiwa kuhusu tukio hilo.

Tukio hilo lilitokea tarehe 1 Aprili mwaka huu katika mazishi ya Mzee Jackson Kibori ambapo Odinga alikwenda kushiriki mazishi hayo yaliyofayika katika shamba la Samitui kaunti ya Uasin Gishu.

Inaelezwa kuwa kulitokea kundi la vijana waliopiga mawe helkopta hiyo ya Rais na kuharibu mifumo ya hewa sambamba na kuvunja vioo vya gari lake.

Aidha, baada ya tukio hilo, mpizani wa Raila katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyka Agosti mwaka huu, Naibu Rais William Ruto alilaani uhalifu huo na kuagiza vyombo vya usalama kuwachukulia hatua wote walioshiriki.

Aidha, wabunge hao ambao wanatajwa kuwa na ukaribu na Ruto wamekanusha kuhusima katika vurugu hizo.

Walisema kuwa wako tayari kuandika taarifa kwa ofisi za DCI ili kuthibitisha hawakuhusika na kisa hicho.

“Tuko tayari kubeba mzigo huo, tupo kwa ajili ya haki, tunahubiri amani siku zote, tunaelekea Nakuru kwenda kusikiliza upuuzi huu, ni upuuzi mtupu, chochote wanachotaka kufanya tuko tayari kwa hilo.

“Kama wanasiasa, tunapaswa kuacha kuajiri wahuni ili kuwasumbua wengine hata kwenye mazishi. Sio Waafrika,” wamesema.

Aidha, wamedai kushangazwa na hatua ya kuhojiwa kwao ilihali vijana waliihusika wanafahamika.

Mmoja wa wabunge hao alidai kuwa aliambatana na Raila saa chache kabla ya mazishi ya Mzee Kibor.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!