March 7, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wabunge 19 Chadema kulinda kura Dodoma

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

Spread the love

VIONGOZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamesema watawatumia wabunge kumi na tisa wa chama hicho kulinda kura katika uchaguzi mdogo wa kata ya Kizota katika jiji la Dodoma. Anaripoti Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Viongozi walitoa kauli hiyo jana nje ya ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Kizota muda mfupi baada ya mgombea udiwani kata hiyo kupitia Chadema, Omar Bangababo kurejesha fomu ya ugombea kata hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Katibu wa Chadema Kanda ya Kati, Iddy Kizota amesema watawatumia wabunge wa Chadema kulinda kura za mgombea kutokana na kuwapo kwa hujuma za kuwapiga mawakala na kuwaondoa vituoni kwa lengo la kubadilisha matokeo.

Hata hivyo Kizota amesema kulikuwepo na njama kubwa ambazo zilikuwa zikifanywa na Ofisi Mtendaji wa Kata ya Kizota, Loyce Mrefu kwa kutaka kumkwamisha mgombea wa Chadema kwa kumwekea vikwazo visivyokuwa na sababu.

“Unaweza kujiuliza msimamizi wa uchaguzi anakuwa na visingizio kibao kwa kudai kuwa ofisi ya kata haina daftari ya orodha ya wapiga kura, mara hakuna risiti kwa kwa ajili ya kumpatia mgombea pamoja na mambo kadha wa kadha,” amesema Mrefu.

Amesema kutokana na kuwapo dalili za hujuma ambazo zinafanywa na viongozi wa chama tawala kwa kushirikiana na watumishi wa serikali wamejipanga kuhakikisha wanalinda na kusimamia sheria, kanuni na misingi yote ya uchaguzi.

Hata hivyo Afisa Mtendaji wa Kata ya Kizota, Loyce Mrefu alipoulizwa juu malalamiko ya wanayoelezwa na wanachama wa Chadema alisema yeye siyo msemaji wa uchaguzi ingawa ni Ofasa Mtendaji kata.

Pamoja na kudai kuwa siyo msemaji alieleza kuwa vyama vilivyochukua fomu na kurejesha mpaka ni vyama siasa ni CCM, Chadema, NCCR-Mageuzi, CUF, UDPD na NLD.

Kwa upande wa mgombea udiwani kata ya Kizota kupitia Chadema, Omar Bangababo amesema amenitosa kuwania nafasi hiyo ili kupambana na changamoto ambazo mtangulizi wake ameshindwa kuzitatua kutokana na kukosa msimamo kwa wananchi walio mchagua.

error: Content is protected !!