July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wabrazil kuharibu soko la wachezaji wa Kenya, Uganda

Geilson Santos Santana ‘Jaja’

Mshambuliaji wa Yanga raia wa Brazil, Geilson Santos Santana ‘Jaja’ akiwasili uwanja wa ndege kuitumikia klabu hiyo

Spread the love

NIDHAMU iliyooneshwa na mshambuliaji mpya wa klabu ya Yanga, Geilson Santos Santana ‘Jaja’ inatarajiwa kuwa kigezo cha kuwaadhibu wachezaji goigoi na wachelewaji wa Tanzania na wengine wa kigeni.

Mshambuliaji huyo aliyesajiliwa kutoka Brazil ili kuichezea klabu hiyo katika mechi za Ligi Kuu ya Bara na michuano ya kimataifa msimu ujao alichukua masaa 16 baada ya kutua nchini na kuanza mazoezi na wenzake.

Kitendo hicho ni kigumu sana kufanywa na wachezaji wanaotoka katika nchi za Afrika Mashariki kwani mara nyingi huwachukua siku mbili hadi tatu kuanza mazoezi kwa kisingizio cha uchovu wa safari. Vilevile, baadhi yao hujikokota sana kufika uwanjani kwa ajili ya mazoezi.

Jaja ni mchezaji wa pili kutoka Brazil kusajili katika kikosi hicho kinachonolewa na Mbrazil, Marcio Maximo akisaidiwa na Leonaldo Leiva. Mchezaji mwingine kutoka Brazil ni kiungo mshambuliaji Andrey Coutinho ambaye alikwishaanza mazoezi.

Kwa muda mrefu Yanga imekuwa ikisumbuliwa na wachezaji wawili wa Uganda Hamis Kiiza na Emmanuel Okwi. Kwa mfano, Okwi amekuwa msumbufu katika klabu zote alizochezea za Simba ya Dar es Salaam, Etoile du Sahel ya Tunisia, na SC Villa ya Uganda.

Nidhamu ya Jaja na Coutinho inaweza kutumiwa na klabu za hapa nchini kuelekeza macho yao nje ya Afrka na kutosajili wachezaji kutoka Afrika Mashariki yaani Kenya, Rwanda, Burundi na Uganda.

Wachezaji wengine waliowahi kuonesha usumbufu waliposajiliwa na klabu za hapa nchini ni Haruna Niyonzima na Mbuyu Twite wa Rwanda.

Pia, mazoezini, wachezaji hao wamekuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki wanaohudhuria kutokana na namna wanavyopokea mipira, pasi na wanavyopiga mashuti kulenga goli.

Kama wachezaji na makocha hao kutoka Brazil wataendelea na tabia hiyo katika muda mchache wakiwa Yanga ni wazi watakuwa wameua soko la wachezaji wa Afrika Mashariki ambao wamekuwa wasumbufu.

Lengo la Shirikisho la Soka Tanzania kuruhusu klabu kusajili wachezaji wa kigeni ni kuwapa changamoto wachezaji wazawa kwa kuongeza ushindani ndani na nje ya uwanja. Badala yake wachezaji wa Afrika Mashariki wamekuwa kero.

 

error: Content is protected !!