August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Wabaya’ wa Dk. Shein wadakwa

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein

Spread the love

WASIOPENDA kusikia jina la Dk. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar kwa mujibu wa makubaliano ya uongozi wa msikiti wao, sasa wamekamatwa, anaandika Mwandishi Wetu.

Waliokamatwa na Serikali ya Dk. Shein wanatajwa kuwa wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF) ambao ni waumini wa Msikiti wa Kijiji cha Kangagani, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Ijumaa ya wiki iliyopita kwenye msikiti huo kuliibuka mgogoro baada ya mtoa mawaidha wakati wa Swala ya Ijumaa kutaja jina la Dk. Shein kinyume na makubaliano ya waumini wa msikiti huo waliopiga marufuku kutajwa jina hilo.

Wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi ni Salum Hamda Simba (37), Jamal Hamdi Khatibu (40), Khatib Jamal Jabu (62) na Ali Dogi (44).

Haji Khamis Haji, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba amethibitisha kukamatwa kwa watu hao.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa, waumini wa msikiti huo walikubaliana kutotajwa jina la Dk. Shein kwenye msikiti huo kutokana na makovu ya kisiasa yaliyotokea kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita.

Mzozo ulianza baada ya jina la Dk. Shein kutajwa ndani ya msikiti huo huku waumini wakionesha kukerwa kwa mtoa mawaida huyo, taratibu mzozo ukaanza kuibuka.

Hata hivyo, kabla ya vurugu kuwa kuwa, baadhi ya waumini kutokana na kukerwa na jina la Dk. Shein ndani ya msikiti huo, waliamua kutoka nje.

Ilipofika usiku wa saa tatu, Jeshi la Polisi lilivamia msikiti huo uliogomea kutajwa jina la Dk. Shein na kuanza kupiga mabomu.

Baada ya polisi kuvamia na kupiga mabomu, hali ya taharuki ilitanda na kusababisha watu wanaoishi jirani na msikiti huo kuanza kukimbia.

Said Ahmad Muhammad, Ofisa wa Ofisi ya Mufti wa Taasisi ya Kiislam anayeshughulikia Fatwa (maamuzi) alinukuliwa akisema, kuwa mgogoro kwenye msikiti huo anaujua.

Na kwamba, pande hizo zilieleza umuhimu wa kutuingiza masuala ya kisiasa kwenye nyumba za ibada.

Hata hivyo, baada ya pande hizo mbili kuelezwa umuhimu wa kutenganisha siasa na ibada, walikubaliana kuwa Dk. Shein hatotajwa tena kwenye msikiti huo na kuwa, alishangaa jina hilo kutajwa kinyume na makubaliano.

error: Content is protected !!