July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waathirika wa ajali fungueni kesi-Serikali

Moja ya ajali ya basi, iliyosababisha vifo na ulemavu wa abiria wake

Spread the love

SERIKALI imesema wale wote wanaopata ajali wakiwa katika vyombo vya makampuni ya usafirishaji, wana uwezo wa kufungua mashauri ya madai ndani ya miaka mitatu tangu kupata ajali hiyo. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereila Ame Silima,ametoa ufafanuzi huo bungeni wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kibaha Mjini, Silvestry Koka (CCM).

Koka katika swali la nyongeza, alitaka kujua serikali inawafidiaje wale wote ambao wanapata ajali wakiwa katika vyombo vya usafiri.

Awali katika swali lake la msingi, Koka alitaka kujua taratibu za kisheria zikoje zinazotakiwa kufuatwa na pande zote zinazohusika na ajali, muda gani unapaswa kupita hadi polisi na mahakama kumaliza tatizo la ajali iliyotokea.

Katikamajibu yake, Silima amesema ndani ya miaka mitatu mtu aliyepata ajali anaweza kufungua shauri la madai kwenye kampuni husika.

error: Content is protected !!