May 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Waandishi watoa ya moyoni siku ya habari

Spread the love

WAKATI Tanzania ikiungana na mataifa mengine duniani wiki hii kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari kauli mbiu ikiwa ‘Kupata Taarifa ni Haki yako ya Msingi:Idai,’ haya ni maoni ya baadhi ya waandishi wa habari waliofanya mahojiano na MwanaHALISI Online, anandika Pendo Omary.

Francis Godwin – Mmiliki wa blog ya Matukio Daima na mwandishi wa gazeti la Jambo leo mkoni Iringa. “Huu ni uhuru wa kuzaliwa nao. Sheria zote zinazotungwa zinapaswa kuzingatia haki hiyo. Miaka 15 iliyopita Tanzania ilikuwa na Sheria 16 zinazominya uhuru wa habari. Hivi sasa sheria hizo zinaongezeka hadi kufikia 26 na serikali iko mbioni kupeleka nyingine Bungeni.

Wanahabari na wadau wake tukikubali serikali iendelee kutuletea sheria za aiana hiyo tutakuwa tunakubali kujenga ukuta wa kuzuia upatikanaji na uzasambazaji wa habari. Tunaomba serikali izingatie maoni ya wadau wa habari wakati ikitunga sheria hizo.”

Said Michael – Machora katuni gazeti la MTANZANIA kila siku na Shirika la Utangazaji la Ujerumani Deutsche Welle (DW). “Hakuna uhuru wa habari hapa Tanzania, Kinachofanyika ni ujanja flani wa watawala kutumia maneno mataamu ya uongo yenye vionjo vya ukweli ili mataifa makubwa yaamini Tanzania kuna uhuru wa vyombo vya habari.

“Hakuna asiyejua waandishi wa habari wanakufa kama si kimwili basi wanakufa moyo wa kufanya kazi kutokana na mazingira magumu yaliyowekwa na kuendelea kutumiwa na watawala.”

Juma Mtanda– Mwandishi wa gazeti la Mwananchi. “CHA msingi viongozi katika idara mbalimbali serikalini, taasisi binafsi za zile za serikali wajitahidi kutoa ushirikiano kwa waandishi pindi wanapohitaji ufafanuzi wa jambo fulani ama ‘kubalance’ kwani mwandishi anapomfuata kiongozi ktk maeneo hayo tayari ana jambo ambalo anajua au amesikia. Pengine malalamiko fulani na hapo kuna ulazima wa kiongozi huzika kutolea ufafanuzi

“Moja ya faida kwa kiongozi kutoa ushirikiano au ufafanuzi wa jambo fulani kwa mwandishi kunasaidia kufuta kauri au kujibu shutuma zinazotolewa upande la mlalamikaji ambazo kwa namna moja ama nyingine husaidia msomaji kupata ukweli wa habari iliyoandikwa.”

Grace Semfuko – STAR TV. “ Wamiliki wa vyombo vya habari wanapaswa kuangalia maslahi mapana ya waandishi wa habari. Habari nyingi zinazoandikwa ni kama matangazo. Zikiwa na lengo la kusifia taasisi au mtu bila kujali uandilifu wake. Kwa mfano ukifungua vituo vya; ITV, STAR TV, TBC na CLUDS TV habari zinazotangazwa kwa asilimia kubwa zinafanana.

“Tungekuwa na vitendea kazi bora, usafri na maslahi mazuri tungeweza kwenda popote na kuandika habari kwa maslahi ya wananchi.”

error: Content is protected !!