January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waandishi wapigwa msasa kuelekea Uchaguzi

Spread the love

WAANDISHI wa habari nchini wametakiwa kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari za uchaguzi wa kidemokrasia ili kulinda amani na utulivu. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Wito huo umetolewa na Mwezeshaji wa Mafunzo kwa Waandishi wa Habari jinsi ya kuandika habari za Uchaguzi, Kaanaeli Kaale katika Mikoa ya Iringa, Morogoro, Pwani na Dodoma.

Katika semina hiyo iliyoendeshwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC nwakishirikiana na Baraza la Habari Tanzania (MCT).

Kaale amesema waandishi wanapaswa kuwa na weledi katika kuandika habari hizo ili waweze kutumia taaluma yao kuifikia jamii.

“Vyombo vya habari ni mshipa mkuu wa damu katika moyo wa demokrasia na pia waandishi ndio wanaosaidia kukuza demokrasia nchini, ni vyema zikaandikwa habari kwa kuzingatia maadili,” amesema.

Aidha amesema ni vyema waandishi wakazingatia maadili ili kuepuka kuliingiza Taifa katika vita ya wenyewe kwa wenyewe kwa uandishi propaganda.

Kwa upande wake Mwezeshaji mwingine Hassan Mhelela, amewataka waandishi kufuata sheria juu ya anayepaswa kutangaza matokeo ya uchaguzi badala ya kutangaza matokeo kutoka kwa watu wasiokuwa na uhakika na wasiotambulika kisheria.

Mhelela ametolea mfano kilichotokea nchini Kenya baada ya kutofuata sheria, hali iliyosababisha kuishia katika maeneo mabaya ni vyema kuepukana na chuki, uchochezi na upiga debe.

error: Content is protected !!