Monday , 11 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Waandishi waombwa kuwa mabalozi wazuri wa TMA
Habari Mchanganyiko

Waandishi waombwa kuwa mabalozi wazuri wa TMA

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk.Ladislaus Chang'a
Spread the love

 

KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk.Ladislaus Chang’a amewaomba waandishi wa habari kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa Mamlaka hiyo huku akiwataka kuweka mkazo katika umuhimu wa matumizi ya taarifa za hali ya hewa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza Jana jijini Dar es Salaam katika warsha ya wanahabari kuhusu mwelekeo wa msimu wa mvua za Vuli kwa kipindi cha mwezi Novemba 2023 hadi Aprili 2024 alisema utoaji wa taarifa kwa jamii unasaidia kwa kiasi kikubwa jamii katika shughuli zao za Kila siku.

Alisema warsha hii ni muendelezo wa juhudi wa warsha zingine na hususani ya hivi karibuni ya mvua za msimu wa Vuli 2023 lengo likiwa kuendelea kuhakikisha taarifa za hali ya hewa zinawafikia walengwa ikiwemo jamii kwa uhakika wa usahihi zaidi.

Dk. Chang’a alisema taarifa za hali ya hewa zikiifikia jamii kwa haraka ,uhakika na usahihi itasaidia jamii kukabiliana na changamoto za Mabadiliko ya Hali ya hewa.

Dk. Buruhani Nyenzi, Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)

“Taarifa hizi zinasaidia Mamlaka kupanga mipango ya kukabiliana na majanga yatokanayo na Hali mbaya ya hewa , upatikanaji wa Chakula na Lishe Bora pamoja na Afya kwa Ustawi wa Jamii,” alisema.

Alisema Mamlaka yao inahusika kutoa tahadhari za majanga yatokanayo na hali mbaya ya hewa yanayoathiri watu na mali zao.”majanga haya ni pamoja na mvua kubwa ,joto/baridi Kali ,upepo mkali na mawimbi makubwa baharini na ziwani pamoja na tahadhari za Tsunami,”alisema na kuongeza

“Hali hii inaleta Changamoto kubwa kwa wananchi hususani wakulima, wavuvi, wafugaji, wasafirishaji, wajenzi, wachimbaji madini na sekta nyingine mbalimbali za kijamii na kiuchumi,” alisema.

Dk. Chang’a alisema wanaendelea kutoa elimu kuhusu msimu unaendelea wa Oktobar hadi Disemba 2023 ambao walitabiri uwepo wa mvua za juu ya wastani kutokana na hali ya El-Nino.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Kesi ya mfanyakazi wa CRDB itaendelea J’tatu

Spread the love  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam inatarajia...

Habari Mchanganyiko

Mawasiliano Dar – Bagamoyo yarejea

Spread the loveMAWASILIANO ya barabara ya Mkoa wa Pwani na Dar es...

Habari Mchanganyiko

Tanesco: Mvua chanzo kukatika umeme leo

Spread the loveShirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limedai kuwa hitilafu iliyojitokeza katika...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Zara tours yajivunia kupandisha wageni 228 Mlima Kilimanjaro

Spread the loveKampuni ya utalii ya Zara tours ya mjini Moshi mkoani...

error: Content is protected !!