WAANDISHI wa habari wawili wa mtandao wa Reuters wa Lone na Kyaw Soe Oo, wamehukumiwa kifungo cha miaka saba jela na Mahakama nchini Myanmar, kwa kosa la kufanya uchunguzi wa siri katika taifa hilo kuhusu mgogoro wa Rohingya. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).
Lone na Soe Oo walishikiliwa kwa kosa la kuwa na nyaraka za serikali ambazo zilizodaiwa kutolewa na askari polisi .
Kabla ya hukumu hiyo, katika utetezi wao waandishi hao walijitetea kwamba waliwekewa mtego na vyombo vya dola kwa kupewa nyaraka hizo nyeti za serikali na askari polisi ili ziwatie hatiani.
Hukumu hiyo imepingwa na watu wengi kwa kuwa imelenga kuminya uhuru wa habari nchini humo.
Leave a comment