September 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Waandishi wa habari watano wakamatwa na Taliban

Spread the love

 

Zaidi ya waandishi wa habari watano kutoka gazeti maarufu la uchunguzi la Etilaatroz ambalo hutoka kila siku huko Kabul nchini Afghanistan wamekamatwa na wanamgambo wa Taliban.

Wanagambo hao wa Taliban wamechukua madaraka tarehe 15 Agosti mwaka huu na kutangaza kuunda serikali.

Kwa mujibu wa Mhariri Mtendaji wa gazeti hilo, Zaki Daryabi amekieleza kituo cha runinga cha Tolo news kwamba Taliban walimkamata mpiga picha aliyekuwa anachukua matukio kwenye maandamano yaliyoibuka katika mji Kabul.

Aidha, kituo hicho cha runinga nacho kimesema mpiga picha wake mmoja aliyefahamika kwa jina la Wahid Ahmadi naye anashikiliwa na wanamgambo wa Taliban ambao wameichukua pia kamera yake.

Aidha, katika vurugu zilizoibuka kwenye mji huo wa Kabul mapema wiki iliyopita, baadhi ya waandamanaji walitawanyika baada ya Taliban kupiga risasi za moto hewani.

Tukio hilo lilitokea baada ya mamia ya Waafghanistan kuandamana hadi ubalozi wa Pakistan nchini humo kupinga Kikundi kingine cha wanamgambo wenye itikadi kali kutoka Pakistan ambacho kina ushirika wa karibu na Taliban.

Kikundi hicho ambacho kinatafsiriwa kuwa cha kigaidi kinafahamika kama Tehreek-i-Taliban Pakistan (TTP), huku kikiwa na malengo ya kuhakikisha Pakistan na Afghanistan zinakuwa nchi zinazoongozwa kwa misingi ya sharia za kiislamu.

Ujio wa kikundi hicho nchini Afghanistan, uliibua hasira za wanaharakati wanaopinga itikadi zake nchini humo.

TTP kilitoa onyo kwa wanahabari na wanaharakati wanaowapinga na kuwaita kuwa ni kikundi cha kigaidi.

Msemaji wa TTP, Mohammad Khurasani mapema wiki hii amesema walikuwa wakifuatilia taarifa za habari ambazo zilidai kuwa kikundi hicho ni cha kigaidi kutokana na misimamo mikali ilichonacho.

error: Content is protected !!