
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan
WAANDISHI wa habari wanne kutoka vyombo mbalimbali vya habari, ni miongoni mwa Wakuu wa Wilaya (DC) 139, walioteuliwa na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Uteuzi huo, umefanywa na Rais Samia jana Jumamosi, tarehe 19 Juni 2021.
Waandishi hao wa habari ni; Abdallah Mwaipaya wa Kituo cha Televisheni na Redio (ITV na Redio One), ambaye ameteuliwa kwenda Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro.
Mwingine ni; Fatma Nyangasa wa Azam Media, aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Mkoa wa Dar es Salaam.
Pia, Gabriel Zakaria wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mkoa wa Simiyu na Simon Simalenga wa Clouds, ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Songwe.
More Stories
CCM yataka viingilio Sabasaba vipunguzwe
Mahakama yasema uamuzi kesi ya kina Mdee haujakamilika
Mbivu, mbichi kesi ya kina Mdee kujulikana leo