Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Waandishi Afrika watakiwa kuweka kumbukumbu sahihi 
Habari Mchanganyiko

Waandishi Afrika watakiwa kuweka kumbukumbu sahihi 

Simon Mkina, Rais wa Taasisi ya Waandishi wa Habari Tanzania (Tajoa), akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka katika nchi za Bara la Afrika
Spread the love

WAANDISHI wa habari Afrika, wamehimizwa kuandika kwa usahihi habari zinazohusu bara hilo, ili kuweka kumbukumbu na marejeo kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Anaripoti Mwandshi Wetu, Johannesburg, Afrika Kusini … (endelea).

Akitoa mhadhara jana tarehe 28 Oktoba 2019 jijini Johannesburg, Afrika Kusini, Rais wa Taasisi ya Waandishi wa Habari Tanzania (Tajoa), Simon Mkina alisema, waandishi wengi nje ya Bara la Afrika – mara nyingi, wamekuwa wakiandika kwa kupotosha habari zinazohusu maendeleo, watu, mazingira na masuala mengine ya bara hilo.

Katika mhadhara huo, unaohudhuriwa na waandishi wabobezi wa habari za uchunguzi Afrika, unafanyika katika Chuo Kikuu cha Witwatersrand, Mkina alisema wakati umefika sasa kwa waandishi hao kuunganisha nguvu ili kuwa na sauti ya pamoja kujenga taswira sahihi ya Afrika.

“Nguvu ninayohimiza hapa ni kuandika mazuri, kuitetea kwa wale wanaoposha habari zake na kuanika mabaya yanayofanywa na baadhi ya Waafrika kulingana na nafasi na dhamana walizonazo katika jamii,” alisema.

Mkina alisema, nguvu ya pamoja kuandika kuhusu Afrika, haina maana ya kuficha maovu na mabaya, ila ni kuyaweka kwa usahihi na siyo kuyakuza wala kupotosha, na kuyafanya matukio hayo kuwa jumuishi kwa kila nchi.

Alisema, habari nyingi zinazoandikwa na vyombo vya habari nje ya Afrika, vinajumuisha kila tukio la baadhi ya nchi ya Afrika kuwa la bara zima.

“Kuna matukio kwa baadhi ya nchi za Afrika kuwa na viongozi wanaopenda kung’ang’ania madaraka, kukumbatia rushwa, kuonea raia, kuminya demokrasia na kudhibiti vyombo vya habari, sasa wenzetu nje ya bara hili wakiandika, wanapotosha kana kwamba matukio ya namna hiyo, yapo kwa kila nchi ya Afrika, jambo ambalo siyo sahihi,” amesema.

Mkina alitumia mhadhara huo kukumbusha umuhimu wa vyombo vya habari kwa maendeleo ya Afrika na watu wake na kwamba, bila vyombo vya habari makini na vyenye uzalendo kwa bara hilo, historia iliyondikwa wakati wa ukoloni kuhusu bara hilo, itaendelea kujirudia.

Mhadhara huo wa siku tatu, unahudhuriwa na waandishi wabobezi wa habari za uchunguzi wa Afrika unamalizika kesho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!