June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waandishi 53 kuchuana EJAT

Makamo wa Rais wa Tanzania, Dk. Gharib Bilali

Spread the love

BAADA ya uchambuzi wa kazi 959 zilizowasilishwa, hatimaye majaji wameteua jumla ya waandishi 53 watakaoingia kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2014, zilizoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT). Anaandika Mwandishi Wetu… (endelea)

Makamu wa Rais Dk. Mohamed Ghalib Bilali ndiye anatarajia kuwa mgeni rasmi
wakati wa kukabidhi tuzo hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Mwenyekiti Kamati ya Maandalizi ya EJAT 2014, Kajubi Mukajanga, amesema tuzo hizo zitafanyika Aprili 24 mwaka huu.

Amesema “tuzo hizo zinafanyika wakati jopo la majaji tisa likiongozwa
na Jaji Mkuu, Chrysoston Rweyemamu, limemaliza kazi yake ya kuchambua
kazi zilizowasilishwa na waandishi kwa ajili ya kushindania makundi 21.

Mkoa wa Dar es Salaam unaongoza kwa waandishi kuwasilisha kazi 412
wakifuatiwa na Mwanza ambao wamewasilisha kazi 198, Kagera umeshika
nafasi ya tatu kwa kuwa na kazi 66 , Zanzibar ipo nafasi ya nne wakiwa
na kazi 46, huku Arusha ikishika nafasi ya tano kwa kuwa na kazi 37.

Kazi hizo zimewasilishwa na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya
habari 69, lakini Kajubi anasema idadi hiyo imepungua kwa silimia 47 ikilinganishwa na wateule 101 waliopatikana mwaka jana.

“Wakati mwaka jana idadi ya wateule wa EJAT wanawake iliongeza kutoka
11 hadi 18, kwa mwaka huu, imeshuka kwa asilimia 38.8,”amesema Kajubi.

Amesma kuwa sambamba na EJAT, pia jopo la wataalam la Tuzo
za Maisha ya Mafanikio katika Uandishi wa Habari (LAJA), wamewasilisha
majina ya wateule ambao watatangazwa wakati wa hafla ya tuzo hizo.

Tuzo hizo zinatolewa kwa mara ya sita mfululizo lengo likiwa ni kuongeza ari, uwajibikaji na kufuata maadili katika kazi ya uandishiwa habari na utangazaji.

error: Content is protected !!