January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waandamana wakihofia kipindupindu

Spread the love

WANANCHI wa Mtaa wa Mkuyuni Sokoni, kata ya Mkuyuni Wilaya ya Nyamagana, jijini Mwanza, wameandamana na kufunga mtaa huo, wakiishinikiza serikali kuondoa dampo la taka wakihofia ugongwa wa milipuko wa kipindupindu. Anaandika Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Hali hiyo imekuja ikiwa ugongwa wa kipindupindu ukiwa umeshamili katika baadhi ya mikoa hapa nchini, ikiwamo Mkoa wa Mwanza ambao zaidi ya watu 17 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.

Wakizungumza na gazeti hili juzi, wananchi hao walisema, halmashauri inapaswa kuhakikisha inalihamisha dampo hilo ambalo limekuwa mahali hapo kwa muda wa miezi mitatu bila kutolewa na kusababisha harufu mbaya na milipuko ya ugonjwa kwa wakazi wa eneo hilo.

Wamesema kuwa usalama wa afya zao zipo hatarini kutokana na uchafu uliokithiri eneo hilo, hivyo ni bora uongozi wa halmashauli ya jiji ikachukua hatua za haraka ili wananchi kuepukana na ugonjwa huo.

Mmoja wa wananchi hao, Delila Ulimboka, eneo hilo la dampo limekuwa likitoa halufu chafu na wakati wa mvua limekuwa lilitililisha maji na kuingia katika makazi ya watu kitendo ambacho ni hatari kwa usalama wa afya zao.

“Tunaiomba halmashauri ya jiji lichukue hatua mapema na namna ya kuhamisha dampo kwani lipo kwenye makaziya watu na eneo la biashara za watu, na watu wanaofanya biashara hapa wanatoka sehemu mbalimbali hivyo kipindupindu kikiingia hakitaathiri watu wengi,” amesema Ulimboka.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Mkuyuni Sokoni, Godwill Kyangala, amesema, kipindi cha nyuma dampo hilo lilikua eneo la soko hivyo lilihamishwa na baadhi ya viongozi ambao hakuwataja majina yao kwamba na kujenga nyumba.

Amesema, awali wakati dampo hilo linahamishwa walidai litakuwa eneo hilo kwa muda lakini hadi sasa halijaondolewa hivyo limekuwa kero kwa wananchi wa mtaa huo kutokana na kuwepo katika eneo la makazi ya watu.

Aidha aliwaomba viongozi wa afya wa jiji kuangalia utaratibu wa kuhamisha dampo hilo ili kuweza kuepukana na ugonjwa wa milipuko yanayoweza kutokea.

Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Jeremia Mahinya, alipotafutwa na gazeti hili kuzungumzia suala hilo, simu yake ya mononi haikuweza kupatikana.

error: Content is protected !!