Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Waajiliwa wa CCM wajilipa Mil 270 kabla ya wakati
Habari za SiasaTangulizi

Waajiliwa wa CCM wajilipa Mil 270 kabla ya wakati

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Dk. Edmund Mndolwa
Spread the love

JUMUIYA ya Wazazi Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Morogoro imewasimamisha kazi mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Mkono wa Mara, Rajabu Vindili na Mhasibu wake Hamisi Kiula kwa tuhuma za ubadhirifu zaidi ya Sh. 270 milioni baada ya kujilipa mishahara ya miezi 18 pamoja na kukusanya fedha kwa kutumia akaunti za miamala ya simu zao binafsi. Anaripoti Christina Haule … (endelea).

Katibu wa Jumuiya hiyo ambayo ndio wamiliki wa shule hiyo Selemani Pinde amechukua hatua hiyo baada ya kupokea taarifa ya Tume iliyotumwa kuchunguza hali ya sintofahamu iliyokuwepo kwenye shule hiyo  na kugundua kuwa waahiriwa hao wamejilipa mishahara kabla ya wakati kuanzia mwezi Januari 2018 hadi Juni 2019.

Pinde amesema kuwa kusimamishwa kwa walimu hao kunafuatia uchunguzi ambao utahusisha wakaguzi kutoka makao makuu kukagua hesabu za shule, mashamba ya shule pamoja na wanafunzi ili kuweka nidhamu ya ukusanyaji wa fedha.

Amesema pia wafanyakazi hao wamesimamishwa kazi kufuatia ripoti hiyo kuonesha mwenendo mbaya wa shule hiyo ambayo inauwezo wa kuchukua jumla ya wanafunzi 1,000 wa kitado cha kwanza hadi cha Nne lakini kwa sasa imebaki na wanafunzi 89 tu na kuilazimu Jumuiya ya wazazi kuunda tume kuchunguza undani wa changamoto hizo.

Herry Hoza ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi CCM mkoa wa Morogoro, amesema Jumuiya hiyo haitaweza kukaa kimya ikiangalia shule za Jumuiya hiyo zikiteketea kwa ubadhilifu wa fedha huku taarifa ya fedha ikisoma hakuna hela za kuendesha shule.

Hoza amesema kuwa uongozi huo uliamua kuweka watia saini wawili ili kujinufaisha kufuatia kuwa shule yenye kidato cha kwanza hadi cha nne ina watia saini wawili jambo ambalo halifanani na uhalisia wa suala zima la elimu huku akisema hata vikundi vya Vikoba huwa na watia saini zaidi ya wawili.

Awali Mwenyekiti wa tume hiyo, Milikiel Mahiku amesema ipo haja kwa Jumuiya kuchukua hatua za haraka kwani imebainika hakuna hata fedha za kuanzia kwa matumizi ya shule ukizingatia kuwa shule imekaribia kufunguliwa.

Hata hivyo uchunguzi wa tume hiyo pia umebaini kuwa kwa kipindi cha miaka nane mfululizo, shule hiyo haikuwa na matokeo mazuri kwenye mitihani ya kitaifa hali iliyotajwa kusababishwa na kukosekana kwa usimamizi mzuri.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!