August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waadventista wachangia chupa 253 za damu

Spread the love
KANISA la Waadventista wa Sabato mkoani Dodoma leo limechangia chupa 253 za damu katika kitengo cha damu salama Kanda ya Kati, anaandika Dany Tibason.
Akizungumza na mtandao huu Bunga Dettu, mchungaji wa kanisa hilo amesema, hatua hiyo imefikiwa kutokana na kuwepo kwa uhaba mkubwa wa damu katika hospitali na vituo vya afya moani humo.
Amesema, kanisa hilo kila mwaka Machi 3 huadhimisha matendo ya huruma duniani kote na kwamba, kutokana na umuhimu wa siku hiyo limeamua kutekeleza matendo ya huruma katika hatua tatu kuelekea kilele cha siku hiyo.
Ametaja hatua hizo kuwa ni kutoa damu, kutembelea Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Hospitali ya Manispaa na kutembelea vituo vya watoto yataima na wanaoishi katika mazingira magumu.
Akizungumzia utoaji wa damu amesema wakati wa utumishi wa Bwana Yesu, (Yesu) alikutana na mtu ambaye alimwambia;
“Nilikuwa na njaa ukanilisha, nilikuwa na kiu ukaninywesha na nilikuwa uchi ukanivisha na ndipo mtu huyo akamuuliza Yesu ni lini nilifanya hivyo? Yesu akajibu ulivyowafanyia wale walio wadogo ulinifanyia mimi.”
Dk. Josiah Tayali, Mkurugenzi wa Idara ya Afya Jimbo la Mashariki mwa Tanzania Kanisa la Waadventista amesema uchangiaji wa damu ni jambo muhimu na linadumisha upendo katika jamii.
error: Content is protected !!