Tuesday , 30 May 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Wa-Sudan waling’ang’ania jeshi, kiongozi wa Mapinduzi naye ang’olewa
KimataifaTangulizi

Wa-Sudan waling’ang’ania jeshi, kiongozi wa Mapinduzi naye ang’olewa

Spread the love

WAZIRI wa Ulinzi wa Sudan, ambaye Ijumaa ya tarehe 12 Aprili 2019, aliapishwa kuwa kiongozi mpya wa nchi hiyo, kuchukua nafasi ya Rais Omar al-Bashir, hatimaye amejiuzulu. Anaripoti Saed Kubenea … (endelea).

Awad Ibn Auf, alitangaza uamuzi huo jana Ijumaa, kupitia televisheni ya taifa. Nafasi yake imechukuliwa na Jenerali wa jeshi anayeheshimika, Luteni Jenerali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan.

Mkuu huyo wa baraza la kijeshi amejiuzulu siku moja baada ya kuongoza mapinduzi yaliyomuondoa madarakani al-Bashir, kufuatia wimbi la maandamano ya kupinga utawala wake.

Kuanguka kwa Rais Bashir kulifuatia maandamano na vurugu zilizoanza Desemba mwaka jana. Madai makubwa ya waandamanaji wakati huo, yalikuwa kupanda kwa bei za bidhaa, hasa vyakula na mafuta.

Akitangaza uamuzi wake wa kujiuzulu, Awadh Auf alisema, “ninaachia wadhifa huu kwa maslahi ya taifa.”  Akaongeza, “taifa hili lina watu wazuri na jeshi la kuaminika. Nina imani kwamba makundi hayo mawili yatafanya kazi pamoja.”

Awadh Auf amesema, “ili kuhakikisha kunakuwepo na maelewano ya mfumo wa usalama, na hususani kwa majeshi na kwa kumtegemea Mungu; ngoja tuanze njia ya mabadiliko.” 

Mapema jana, jeshi liliwahakikishia raia kuwa halina mpango wa kuongoza kwa muda mrefu. Lilisema utawala wa kijeshi wa miaka miwili ya mpito unaweza kubadilishwa na kuahidi kwamba linaweza kuvunjwa muda mfupi ujao, iwapo kutafikiwa suluhu la mzozo wa kisiasa unaolikabili taifa hilo. 

Awadh Ibn Auf alikuwa mkuu wa ujasusi katika jeshi la Sudan, wakati wa mzozo wa jimbo la Darfur ulioibuka mwaka 2000. Marekani ilimuwekea vikwazo mwaka 2007.

Jeshi la Sudan lilifanya mabadiliko ya uongozi jana Ijumaa baada ya Jenerali Awad ibn Ouf aliyeapishwa kuongoza baraza hilo la mpito kujiuzulu, siku moja baada ya kuchukua wadhifa huo. 

Maelfu ya wandaamanaji walishangilia mitaani kujiuzulu kwa Jenerali huyo; waandamanaji walikataa uongozi wake kwa maelezo kuwa alikuwa mkuu wa idara ya ujasusi ya kijeshi wakati wa kampeni katili ya kukabiliana na uasi kwenye jimbo la Darfur mwanzoni mwa miaka ya 2000. 

Hata hivyo, pamoja na mabadiliko hayo, waandamanaji wamesema, hawatoondoka mitaani hadi raia watakapokabidhiwa uongozi wa kipindi cha mpito. Wanadai kuwa uongozi wa kijeshi, ni muendelezo wa utawala wa Al Bashir.

Chama cha wasomi wa Sudan, ambacho ndiyo waratibu wa maandamano hayo, kimetangaza kuwa mgomo wa kuketi mbele ya makao makuu ya jeshi utaendelea.

“Tunaowatolea wito wanajeshi wote kuhakikisha kwamba wanakabidhi mamlaka kwa serikali ya kiraia,” taarifa ya chama hicho iliyotolewa kupitia ukurasa wake wa Facebook ilieleza.

Aidha, kimetoa wito wa kuondolewa kwa “maamuzi dhalimu ya viongozi ambao hawawakilishi watu ” na kuondolewa kwa “nembo zote za utawala ulioondolewa mamlakani ambao ulihusika katika uhalifu dhidi ya binadamu.”

“Hadi madai haya yatakapotimizwa tutaendelea na maandamano yetu ya kuketi chini kwenye makao makuu ya jeshi,” ilisema ripoti ya chama hicho cha wasomi wa Sudan.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Mkutano wa Quad Hiroshima waibuka na kutafuta amani na ustawi wa Indo-Pacific

Spread the love  JITIHADA za mazungumzo ya Pande Nne (Quad), hazikuthaminiwa na...

Habari za SiasaTangulizi

Uamuzi juu ya wakurugenzi kusimamia uchaguzi 13 Juni

Spread the love  MAHAKAMA ya Afrika ya Haki za Binadamu (ACHPR), imepanga...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jeshi la Polisi kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika utafiti

Spread the love  JESHI la Polisi Nchini limesema kuwa katika kukabiliana na...

KimataifaTangulizi

Mtuhumiwa wa mauaji ya halaiki ya Rwanda akamatwa Afrika Kusini

Spread the love  MMOJA wa watuhumiwa wakuu wa mauaji ya Kimbari ya...

error: Content is protected !!