Monday , 26 February 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Vyuo vikuu vya ‘wababaishaji’ kukiona
Elimu

Vyuo vikuu vya ‘wababaishaji’ kukiona

Spread the love

TUME ya vyuo vikuu nchini (TCU), imesema itachukua hatua kali za kisheria dhidi ya vyuo vikuu ambavyo vitatangaza kozi ambazo hazitambuliki na tume hiyo pamoja na Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi (NACTE), anaandika Hellen Sisya.

Akizungumza na wanahabari, Eleuther Mwageni, Kaimu Mkurugenzi wa TCU amevitaka baadhi ya vyuo ambavyo tayari vimeonekana kutangaza kozi zisizotambulika na tume hiyo kuacha mara moja, kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

“Wakiendelea kufanya hivyo, tunafata sheria zetu, tutachukua hatua stahiki ……..kuna adhabu zinatolewa,” amesema Mwageni.

Aidha, Kaimu Mkurugenzi huyo amewataka waombaji wa nafasi za masomo ya elimu ya juu nchini kuomba kozi ambazo zinatambulika na tume hiyo pamoja na NACTE na kuvisisitiza vyuo vikuu kote nchini kudahili wanafunzi wenye sifa na vigezo stahiki katika kila kozi.

Zoezi la uombaji wa vyuo kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na elimu ya juu hapa nchini linatarajia kuanza tarehe 22 Julai, mwaka huu ambapo wahitimu wa elimu ya kidato cha sita pamoja na wahitimu wa ngazi ya stashahada wenye sifa stahiki wataomba kudahiliwa na vyuo vikuu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

Takukuru wambana Mwalimu mkuu, atema bungo

Spread the loveMwalimu Mkuu wa shule msingi Hanihani, kata ya Igunga wilayani...

ElimuHabari za Siasa

Prof Muhongo ataka ubunifu mitaala mipya ya elimu

Spread the loveSERIKALI imetakiwa kuhakikisha  maarifa, ujuzi, uvumbuzi na udadisi vinazingatiwa kwenye...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa saidizi kwa walimu, wanafunzi wenye ulemavu Ilala

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi msaada wa vifaa saidizi kwa walimu...

Elimu

St. Mary’s Mbezi Beach High School yafanya maajabu kidato cha nne

Spread the love  WANAFUNZI waliomaliza  kidato cha nne kwenye shule ya sekondari...

error: Content is protected !!