Friday , 1 March 2024
Home Habari Mchanganyiko ‘Vyombo vya haki viboreshwe, mahabusu wapone’
Habari Mchanganyiko

‘Vyombo vya haki viboreshwe, mahabusu wapone’

Spread the love

FAMILIA tatu mkoani Mtwara zimeiomba Serikali ya Tanzania, kuboresha utendaji wa vyombo vyenye dhamana ya kutoa haki, ili kuondoa changamoto ya watuhumiwa kukaa mahabusu muda mrefu, kwa madai ya upelelezi wa makosa yao kutokamilika. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ombi hilo limetolewa leo Alhamisi tarehe 9 Julai 2020, jijini Dar es Salaam na Tiba Moshi Kasoko kwa niaba ya familia hizo tatu.

Familia hizo zimetoa ombi hilo baada ya ndugu zao, Omar Salum Bumbo (51), Ustadhi Ramadhan Moshi Kasoko(41) na Waziri Suleiman Mkaliganda (33) kusota mahabusu kwa zaidi ya miaka miwili katika Mahabusu ya Gereza la Lilungu mkoani Mtwara kwa madai ya kutokamilika kwa ushahidi wa makosa yao.

Watatu hao walikamatwa katika nyakati tofauti mwaka 2017, ambapo wanakabiliwa na tuhuma za makosa ya ugaidi, katika Mahakama ya Wilaya ya Mtwara.

Akizungumza kwa niaba ya familia hizo, Kasoko ameziomba mamlaka husika kukamilisha taratibu za kisheria ili watuhumiwa hao na wengine walioko mahabusu, mashauri yao yatolewe uamuzi, ili kama wana hatia wafungwe au kama hawana hatia waachwe huru.

“Tunaiomba Serikali ya wanyonge inayosimamia haki ili ndugu zetu na mahabusu wengine mfano wao ambao wanaendelea kukata miaka mahabusu watekelezewe kwa haraka utaratibu wa kisheria ambao ni haki yao,” amesema Kasoko na kuongeza:

“Ili kesi zao zisikilizwe na kama ushahidi haujakamilika wapatiwe dhamana na kama haupo waachiwe huru, kuliko kubaki katika hali ya sasa ambayo inatoa sura ya wazi ya uonevu.”

Hata hivyo, Kakoso amesema suala hilo amelifikisha katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), ambayo ilikiri kupokea faili la watuhumiwa hao, na kuahidi kulifanyia kazi.

” Kabla ya kuzungumza na ninyi wanahabari niliwahi kufika Dodoma kwa DPP, akasema mafaili yao yako kwake akasema yatashughulikiwa,” amesema Kakoso.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Karafuu, Parachichi yawa fursa Morogoro

Spread the loveIMEELEZWA kuwa zao la karafuu ambalo kwa sasa linalimwa pia...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washindi 12 NMB MastaBata na wenza wao wapaa Afrika Kusini

Spread the loveWASHINDI 12 wa kampeni ya kuhamasisha matumizi yasiyohusisha pesa taslimu...

Habari Mchanganyiko

4 wanusurika kifo ajali ya ndege Serengeti

Spread the loveWATU wanne wakiwamo abiria watatu na rubani mmoja wamenusurika kifo...

Habari Mchanganyiko

Mafua yamtesa Papa, afuta mikutano

Spread the loveKiongozi wa Kanisa katoliki duniani, Papa Francis amelazimika kufuta mkutano...

error: Content is protected !!