July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Vyomba vya habari vyakumbushwa wajibu

Spread the love

VYOMBO vya habari nchini vimetakiwa kuhakikisha vinasimamia wajibu wake ili kuhakikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu unakuwa huru na wa haki. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Taasisi ya Utawala Bora (CEGODETA), Thomas Mgawaiya wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu namna ya kuandika na kufuatilia habari za Uchaguzi Mkuu.

Programu ya mafunzo hayo imeandaliwa na Shirika la Habari la Kimataifa la Internews ambapo itadumu kwa muda wa miezi 18.

“Wajibu huu usiposimamiwa na kutekelezwa ipasavyo, inaweza kusababisha uchaguzi usiwe wa huru na haki. Pia inaweza kusababisha uvunjifu wa amani na utulivu na hatimaye machafuko na vita vya wenyewe kwa wenyewe kama ilovyowahi kutokea kwenye nchi za Burundi, Rwanda na Kenya”, amesema Ngawaiya.

Amesema vyombo vya habari havitakiwi kupendelea au kuvibagua baadhi ya vyama vya siasa na wagombea, kutopokea rushwa, kutoandika habari za uchochezi, chuki na uhasama baina ya vyama vya siasa na wagombea na kutochochea chuki na uhasama baada ya matokeo rasmi kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

“Pia vyombo vya habari vinatakiwa visimame katika kutetea masilahi halisi ya nchi na wananchi na kutochochea wananchi kufanya fujo na vurugu ama kujichukulia sheria mikononi, ” amesema Ngawaiya.

error: Content is protected !!