May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Vyeti feki: Zitto apongeza uamuzi wa Rais Samia

Zitto Kabwe

Spread the love

 

KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amepongeza hatua ya Rais Samia Suluhu Hassan, kuagiza watumishi waliostaafishwa kazi ikiwemo walioghushi vyeti, kulipwa stahiki zao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, jana tarehe 1 Mosi 2021, Zitto amesema hatua hiyo italeta matumaini kwa watumishi hao, hasa watakapopatiwa fedha zao za michango waliyotoa katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

“Uamuzi huu ni muhimu sana kwa Watu ambao walipoteza kabisa matumaini ya Maisha. Angalau kupewa Fedha zao za michango ya Hifadhi ya Jamii ni ahueni kubwa maana mwendazake aligomea hata kuwapa Haki yao hii,” aliandika Zitto.

Mwanasiasa huyo alisema kuwa, alipokuwa Mbunge wa Kigoma Mjini, alipokea malalamiko mengi kutoka kwa baadhi ya watumishi hao wakiomba wapewe michango yao hiyo.

Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania

“Nilipokuwa Mbunge nilipokea malalamiko mengi ya wakazi wa Jimbo langu walioondolewa kwenye utumishi wa Umma kwa kilichoitwa vyeti feki. Hata michango yao waliyochangia kwenye Mifuko ya Pensheni walinyimwa. Ulikuwa ukatili mkubwa sana. Nafurahi kuwa angalau watapata akiba yao sasa,” aliandika Zitto.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi), yaliyofanyika jana jijini Mwanza, Rais Samia aliagiza waajiri wa watumishi wa umma kufuata sheria na taratibu katika kuhitimidhs ajira za waajiriwa wa darasa la saba ns walioghushi vyeti.

“Nawaagiza waajiri kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika kuhitimisha ajira za watu walioajiriwa elimu ya darasa la sabs na wale walioghushi vyeti, najua wako waajiriwa waliostafishwa na kulipwa na wako hawajalipwa kutokana na madai au kisingizo kwamba serikali haijatoa muongozo mahsusi wa kulipa mafao hayo,” alisema Samia na kuongeza:

“Najua wako wasiolipwa, niwaagize waajiri wote waliokuwa na wafanyakazi wa namna hii wafanye kila inavyowekezana kila mtu apate haki yake. Natambua walikuwa wanakatwa kwenye mifuko ya hifadhi, wale wasio na kumbukumbu waziweke vizuri na wale wasiolipwa kwa sababu serikali haijatoa muongozo, muongozo ndio huu sasa.”

Watumishi hao waliondolewa kazini katika Serikali ya Awamu ya Tano, kufuatia sakata la uhakiki wa watumishi wa umma wenye vyeti vya kughushi, lililoibuka 2017.

error: Content is protected !!