CHAMA cha wafanyanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) kimepoteza zaidi ya wanachama 9,000 kufuatia hatua ya kuwaondoa watumishi wenye vyeti feki na walioajiliwa na vyeti vya darasa la saba jambo linawalopelekea kukabiliwa na deni kubwa serikalini sanjari na kurudisha nyuma uendeshaji wa chama hicho, anaandika Christina Haule.
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti chama hicho, Archie Mntambo wakati akizungumza kwenye kikao cha Baraza Kuu Taifa TUGHE kuwa, wimbi hilo la kuondolewa kwa watumishi wenye vyeti feki limesababisha chama hicho kudaiwa na serikali kiasi cha Sh 100 milioni jambo ambalo linaleta utata wa malipo kutokana na mikataba ya awali ya wafanyakazi hao.
Mntambo amesema kuwa zoezi la kuwaondoa wafanyakazi wenye vyeti feki na walioajiriwa na vyeti vya darasa la saba limewakumbwa watumishi wa serikali pekee huku wengi wao wakiwa ni wanachama wa chama cha wafanyakazi wa Serikali na Afya TUGHE.
Aidha Mntambo amesema kuwa chama hicho pia kinaiomba serikali kuangalia namna ya kuwalipa deni wanalowadai la sh 480 milioni ili chama hicho kiweze kujiendesha na kukabiliana na changamoto mbalimbali inazokumbana nazo mpaka sasa ikiwemo kuyumba kwa uendeshaji wa chama kutokana na kupungua kwa wanachama hao.
Naye Katibu wa TUGHE, Herry Mkunda, amewataka wanachama waliobaki kuendelea kukitumikia chama kufuatia chama hicho bado kuwa na nguvu na uwezo katika utendaji unaotokana na viongozi bora waliowachagua.
Kwa upande wake, Kaimu mkurugenzi wa shirika la Bima ya Afya Tanzania (NHIF), Christopher Mapunda, amezitaka hospitali na vituo vya afya vinavyotoa huduma huku kukiwa na malalamiko ya wagonjwa kupewa majibu yasiyosahihi, kubadilika na kutoa huduma bora kwani kufanya hivyo kunaweza kuwaondoa au kuwasitisha katika utoaji huo wa huduma.
Mapunda amesema kuwa kumpa mgonjwa majibu ya vipimo isivyo sahihi husababisha mgonjwa kutumia dawa zisizostahili na kumsababishia usugu mwilini.
Hivyo amesema wanaendelea kufanya utafiti kubaini kama maneno hayo ya ukweli au hayana na kuweza kuchukua hatua stahiki.
Hata hivyo Mapunda aliiomba Serikali kuweka utaratibu mzuri wa kuwepo kwa mdhibiti wa gharama za matibabu na dawa ambayo imekuwa ni changamoto kubwa kufuatia watu binafsi kujipangia bei kiholela jambo ambalo limekuwa kero kubwa kwa wananchi wa hali ya chini kuweza kumudu gharama hizo.
Kuna mantiki gani ya wafanyakazi kukatwa mishahara yao ili kujaza mifuko ya viongozi wao? Tangu lini vyama vya wafanyakazi vikawa lazima kwa wafanyakazi wote? Zamani miaka ya 70 na 80 na 90 sote tulikatwa mishahara kwa ajili ya TANU/CCM. Ndo maana chama dola kikatajirika. Leo tunatajirisha wakuu wa TUGHE na JUWATA. Hata JPM amelikubali hilo. TAKUKURU fanyeni kazi yenu. Na mishahara isikatwe kwa lazima. Uwanachama iwe hiyari ya mtu