May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Vyama vya siasa vyaitwa taasisi ya Mwalimu Nyerere

Mwenyekiti wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Paul Kimiti

Spread the love

 

WATU kutoka vyama vya siasa vya upinzani, wameshauriwa wajiunge na Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere, ili waongeze nguvu katika ulinzi wa haki na amani ya Tanzania. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa leo Alhamisi, tarehe 3 Machi 2022 na Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Paul Kimiti, akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, kuhusu maandalizi ya maadhimisho ya miaka 10 ya kuzaliwa kwa Mwalimu Nyerere, itakayofanyika tarehe 13 Aprili mwaka huu.

Kimiti amesema kuwa, taasisi hiyo siyo ya kisiasa wala ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), bali ni ya watu wa kada zote, ambayo lengo lake ni kufuata misingi ya Mwalimu Nyerere, ya kupigania haki na uongozi bora.

“Bado kuna wengine wanaonewa, bado kuna wengine wana matatizo makubwa sana, lakini tuendelee kupiga kelele usiku na mchana bila kuogopa na taasisi yetu tutasambaa. Si sulaa la siasa hapana, ni misingi iliyotufanya tuishi Pamoja. Ndiyo nmaana tumewaalika hata vyama vingine,” amesema Kimiti.

Mwanasiasaa huyo mkongwe nchini Tanzania, amesema taasisi hiyo ina wanachama wengine ambao sio CCM, akiwemo Katibu Mkuu wa Chama cha ADA-Tadea, John Shibuda.

“Sio CCM tu, wako kina Shibuda wameingia wote. Tunasema kila mmoja atakuwa mwanachama ilimradi akubalia masharti tuliyoweka kwenye katiba yetu,” amesema Kimiti.

Kimiti amesema misingi ya haki na watu iliyoachwa na Mwalimu Nyerere, ndiyo imeifanya amani ya Tanzania idumu.

“Baba wa Taifa alisema asili ya uongozi ni vitu viwili, kwanza haki na pili watu. Hakwenda nje ya hapo, asili ya uongozi wetu ni mambo mawili. Watu ukiwatendea haki bila kubagua na ukitenda haki amani itapatikana. Hayo machahe ndiyo yametufikisha hapa tulipo,” amesema Kimiti.

Naye Katibu Mkuu wa taasisi hiyo, Simon Rubugu, amesema lengo la uanzishwaji wa taasisi hiyo ni kueneza upendo, amani na falsafa za Mwalimu Nyerere.

“Tukaona ni vizuri tukaanzisha taasisi hii, ukiangalia bodi yetu au viongozi wetu wengi wamefanya kazi naye na walikuwa waadilifu, wanamjua alikuwa nani na watatusaidia kufundisha vijana ambao hawamjui. Rai yetu ni kuwaomba watu wajiunge kwa kuwa taasisi hii ni chombo muhimu cha kueneza upendo, amani, falsafa zake,” amesema Rubugu.

Kwa upande wake Mjumbe wa Sekretarieti ya taasisi hiyo, Ummy Wenceslaus, maarufu kama Dokii, amesema taasisi hiyo itasaidia kuimarisha maadili ya viongozi ili wafuate nyayo za Mwalimu Nyerere.

“Madili.mpaka kwenye Serikali yamemomonyoka, kwa maana si maadili ya baba wa taifa, ni muda wetu kupaza sauti ili tuweze kumzungumzia huyu mzee mpaka kizazi kijacho kijue tu alipigania uhuru,” amesema Dokii.

error: Content is protected !!