May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Vyama 11 vyamshukia Askofu Gwajima

Spread the love

 

UMOJA wa vyama 11 vya siasa nchini Tanzania vimemtaka Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kuacha kupotosha umma juu ya corona kwa kuhamisha ugomvi wa kifamilia kwenye masuala ya Kitaifa. Anaripoti Victoria Mwakisimba, TUDARCo … (endelea).

Ni baada ya Askofu Gwajima ambaye pia ni Mbunge wa Kawe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Dar es Salaam kutoa msimamo wa kutochanjwa kwa chanjo hiyo yeye binafsi.

Pia, amewashauri ndugu, rafiki na familia zake anazoziongoza kutokukurupukia chanjo hizo kwani bado hazijathibitishwa.

Uamuzi huo, umemfanya Waziri wa Afya, Dk. Dorothy Gwajima ambaye amekiri hadharani kwamba licha ya Askofu Gwajima kuwa “shemeji yake kabisa” lakini hawezi kuvumilia upotoshaji anaoufanya.

Waziri Gwajima tayari ameagiza jeshi la polisi kumkamata na kumhoji juu ya tuhuma hizo za upotoshaji ikiwemo dhidi ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwamba wamehongwa fedha ili kuruhusu chanjo hiyo kuingia nchini.

Leo Alhamisi tarehe 19 Agosti 2021, vyama 11 vya siasa, vimekutana na wandishi wa habari mkoani Dar es Salaam kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo chanjo ya corona.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Katibu Mkuu wa ADC, Doyo Hassan Doyo amesema, yeye na familia yake tayari wamekwisha kuchanjwa chanjo hiyo na mpaka sasa hakuna madhara yoyote ambayo wamepata.

Amesema, viongozi wa dini zamani waliachwa watengeneze watu kiroho, “lakini utaratibu huu CCM imeuharibu sana.” Hata hivyo, hakufafanua zaidi jinsi ilivyouharibu utaratibu huo.

Wengine sio viongozi wa dini, sisi tunawaomba wawahamasishe wananchi kwenda kuchanjwa kwani chanjo haina madhara yoyote na hao wanaotangaza.

Askofu Josephat Gwajima

Amesema, kauli za Askofu Gwajima “zinachafua wengi, askofu mwaka 2015 wakati wa uchaguzi mkuu alisema chama chake kingepata uraisi angegeuza misikiti kuwa sundayschool. Juzi anagombea ubunge anasema anaitwa Rashid, lakini alisema hataki ubunge leo ni mbunge. Huyu ni mtu wa kumsikiliza kweli? Anapaswa kupuuzwa.”

“Kumbe wakati mwingine ugomvi wa nyumbani unaweza kuhamia serikalini, haya nayo lazima wananchi waelezwe na tuwe makini nao,” amesema Doyo.

Naye Katibu Mkuu wa DP, Abdul Mluya amempongeza Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu kuingia kwa chanjo hiyo kwani amejali maisha ya wananchi ambao anawaongoza na kuwataka wananchi ambao hawajachanjwa kuchangamkia chanjo hiyo.

Vyama hivyo 11 vilivyozungumza; ni DP, NRA, ADC, AAFP,UDP, SAU,UMD,TLP.CCK, NLD na UPDP.

error: Content is protected !!