August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

VVU tishio

Spread the love

MAAMBUKIZI ya Virusi vya Ukimwi (VVU) yanaedelea kuathiri na kutishia maendeleo ya nchi, anaandika Regina Mkonde.

Kutokana na hali hiyo, serikali ina mpango wa kufanya utafiti na kupima wananchi ili kujua namna ya kudhibiti maabukizi mapya.

Hayo yameelezwa leo na Dk. Fatuma Mrisho, Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS) katika kutano wa wadau wa utafiti wa wagonjwa wenye maambukizi mapya ya VVU uliofanyika jijini Dar es Salaam.

“Lengo la kufanyika kwa utafiti ni kuhakikisha kuwa hali ya ukimwi nchini inatambulika pamoja na kujua namna ya kuwasaidia walioambukizwa sambamba na kujua hali za wagonjwa walioambukizwa miaka ya nyuma,” amesema Mrisho.

“Mapambano yetu ni kuhusu maambukizi mapya na ndiyo sababu ya kufanya utafiti na kutoa elimu kwa jamii juu ya kujikinga na maambukizi mapya ili kutekeleza adhimio letu la kutokomeza ugonjwa wa UKIMWI  kwa asilimia mia,” amesema.

Mrisho amesema kuwa ingawa kuliwekwa maadhimio ya kutokomeza ugonjwa wa Ukimwi na kubaki asilimia sifuri ifikapo mwaka 2030, wameamua kuweka malengo ya kupunguza maambukizi, unyanyapaaji na uanzishiwaji wa dawa kwa waathirika wote kwa asimilia 90 kabla ya mwaka 2020 .

“Ni muhimu wakati wote nchi ijue ina hali gani kuhusu wagonjwa wa ukimwi, hadi sasa upimwaji wa ugonjwa huo umekwisha fanywa kwa awamu nne ambapo mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2011/2012 na kwamba kwa mwaka wa 2015/2016 upimaji bado unaendelea,” amesema.

Utafiti huo utafanyika ndani ya miezi miwili kuanzia mwezi Juni hadi Agosti mwaka huu, na kwamba wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano wakati wa utafiti unapofanyika kwa lengo la kuiwezesha serikali kupata takwimu sahihi.

“Awali tulikuwa tunapima watu wanaoanzia umri wa miaka 15 na kuendelea, lakini awamu hii tutapima kuanzia watoto wadogo na kuendelea sababu rika hilo huwa katika hatari ya kupata maambukizi kulingana na njia tofauti,” amesema.

error: Content is protected !!