May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Vuta nikuvute uchaguzi TLS

Dk. Rugemeleza Nshala, Rais wa TLS anayemaliza muda wake

Spread the love

WANACHAMA wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), wamewachambua wagombea urais wa chama hicho kwa mwaka 2021. Anaripoti Regina Mkonde, Arusha … (endelea).

Wanaogombea kiti cha urais wa TLS ni Dk. Edward Hoseah, Flaviana Charles, Francis Stolla, Albert Msando na Shehzada Walli.

Wakizungumza na MwanaHALISI Online leo Alhamisi tarehe 15 Aprili 2021, jijini Arusha, mawakili hao wamesema, uchaguzi wa mwaka huu una mvutano mkali, kutokana na aina ya watu waliojitosa kugombea.

Wamesema, hadi sasa ni wagombea watatu pekee ambao wanaonesha ushindani mkali, tangu wakati wa kampeni hadi leo tarehe 15 Aprili 2021, wakati wa zoezi hilo litakapofungwa.

Wagombea hao ni, Dk. Hoseah, Flaviana na Stolla.

Wakili ambaye hakutaka kutajwa jina kutoka Kanda ya Kaskazini, amesema joto la uchaguzi huo limepandishwa na sababu za kisiasa.

Ameidai, mawakili wenye mlengo wa vyama vya upinzani, wana mtu wao na wale wenye mlengo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wana mtu wao pia.

Wakili huyo amewachambua wagombea hao akisema, Dk. Hoseah anaungwa mkono na wapinzani huku Flaviana akionekana kuungwa mkono chini kwa chini na CCM kwa kuwa, ni mwanachana mwenzao.

“Wapinzani wameweka wazi wanampigia kampeni Dk. Hoseah akiwemo Makamu Mwenyekiti Chadema, Tundu Lissu kasema anamsapoti Hosea, tunajua vijana wenzetu wa upinzani wanamsapoti,” amesema Wakili huyo.

Alipoulizwa nini wapinzani wanamuunga mkono Dk. Hoseah, amesema kutokana na kutumbuliwa kwake katika nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dk. John Magufuli.

Dk Edward Hoseah mgombea Urais TLS

Anasema, Dk. Hoseah ana nafasi kubwa ya kushinda kwa sababu anaonekana ni mtu wa misimamo.

“Kwa nafasi aliyonayo ni rahisi kushawishi. Mfano  mimi nikiuliza sababu ya ushawishi wake ni nini? Ni moja,  Dk. Hoseah alitumbuliwa ns mtu yoyote aliyetumbuliwa na Seriksli anakuwa sapported  na upinzani ikionekana alionewa au alikuwa na misimamo,” amesema.

Kuhusu Flaviana anayesadikika kuungwa mkono na CCM, wakili huyo amesema naye si haba kwani anaweza shangaza watu kwa kuwa CCM wao hufanya kampeni zao chini kwa chini.

“CCM wao hawasemagi hadharani, wanao ona  ni mtu wa upinzani hawampigii hivyo Dk. Hosea hawatampigia ingawa alikuwa serikalini. wanaona wivu.

Shehzada Walli mgombea Urais TLS

CCM  wanaweza msapoti mama (Flaviana) sababu ni mwanachama mwenzao na alishswahi gombea ubunge kwenye kura za maoni, hii inaweza kumsaidia,” amesema.

Naye Wakili Juma Ally, amesema mtu wa tatu anayeleta upinzani katika uchaguzi huo ni Stolla, akisema kwamba ni mtu ansyejenga hoja pia aliwahi kuwa rais wa TLS hivyo ana mtaji wa kutosha.

Hata hivyo, amesema Flaviana naye anaweza kubadili upepo kwa kuwa mwaka huu kuna kampeni ya kuwainua kina mama.

“Stolla nguvu yake iko kwa wanachama humu humu,  urais wake haukua na skendo , Flaviana watu wasimchukulie poa anaweza pindua meza kumbuka ni mwaka wa kina mama,  anaweza suprise mtu,” amesema Ally.

Kuhusu wagombea wengine, Ally amesema Walli hana nguvu sana kwa sababu ni mgeni katika harakati hizo.

“Walli anaungwa mkono na wasio kuwa na  mlengo wowote. Anatafuta wotewote amekuja kama mgombea huru. Possibility ya kushinda hana sababu ni mgeni,” amesema Ally.

Akimchambua Msando, amesema anamtafsiri kama mtu aliyekuja kuchangamsha uchaguzi.

“Hata msando nafasi ya ksuhinda hana. Compition hapo ni Flaviana, Stolla na Dk. Hosea. Msando anachangamsha uchaguzi hawezi kushinda . Hana ushawishi,” amesema Ally.

Walipoulizwa kwamba TLS inahitaji kiongozi wa aina gani, wamesema chama hicho kinahitaji mtu atakayelinda maslahi ya wanachama pamoja na kuimarisha mahusiano ya chama na Serikali, Mahakama na Bunge.

Albert Msando, mgombea Urais TLS

“Tunahitaji kiongizi atakayejenga mahusiano mazuri kati ya TLS na serikali sio kutoka hapa kwenda kudindishiana misuri na serikali. Ajenge mahusiano mazuri kati ya wanachama na Serikali,  Mahakama na Bunge,” amesema Ally.

Uchaguzi wa TLS unatarajiwa kufanyika kesho Ijumaa tarehe 16 Aprili 2021, kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC).

error: Content is protected !!