February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Vurugu zafunga chuo cha Nairobi

Chuo  Kikuu cha Nairobi

Spread the love

CHUO  Kikuu cha Nairobi kimefungwa kwa muda usiojulikana na Wanafunzi chuoni hapo wameamriwa kuondoka chuoni hapo  leo, anaandika Hamis Mguta.

Uamuzi huo umefikiwa na Seneti ya chuo kutokana na suala la kiusalama.

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Umma wa chuo hicho, John Orindi amesema, “Tutatangaza ni lini chuo kitafunguliwa.”

Uamuzi huo umechukuliwa kutokana na maandamano yaliyofanyika wiki iliyopita ambayo yalisababisha wanafunzi 27 kujeruhiwa.

error: Content is protected !!