Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Vurugu, rushwa zatajwa kuahirishwa Mkutano Mkuu TLP
Habari za Siasa

Vurugu, rushwa zatajwa kuahirishwa Mkutano Mkuu TLP

Spread the love

 

KUTAWALA kwa vurugu na rushwa kumetajwa kuwa chanzo cha kutofanyika kwa Mkutano Mkuu wa Chama cha TLP ambao ulikuwa na ajenda ya uchagzui wa viongozi kwa nafasi zilizo wazi ikiwemo nafasi ya Mwenyekiti wa Chama Taifa. Anaripoti Eliabu Kanyika, DSJ … (endelea)

Mkutano huo ulipangwa kufanyika leo Jumatatu tarehe 6 Machi 2023 katika Ukumbi wa ofisi za Makao Makuu ya Chama hicho zilizopo Magomeni jijini Dar es Salaam.

Aklizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuahirishwa kwa mkutano huo Katibu Mkuu wa TLP, Richard Lyimo, amesema uamuzi huo umetolewa na Bodi ya wadhamini wa chama hicho baada ya kujiridhisha kuwa mazingira yaliyopo hayaruhusu kufanyika kwa mkutano huo.

Lyimo, amesema sababu za vurugu zilizofanywa na baadhi ya wajumbe ni kutokana na mkutano kufanyika vyumba viwili tofauti kutokana na ufinyu wa ukumbi ndani ya ofisi hizo za chama.

“Vurugu zimefanywa na baadhi ya wajumbe baada ya kushiriki mkutano huo wakiwa chumba kingine tofauti na viongozi wao sababu ikiwa ni idadi kubwa ya wajumbe walioshiriki mkutano huo,” amesema Lyimo.

“Katika mkutano huo kulitokea vurugu watu kutokuelewana na uongozi kushindwa kumudu hizo vurugu,” ameongeza Lyimo.

Sambamba na hilo Lyimo amezungumzia swala la rushwa kuwa ni chanzo cha kuahirishwa kwa mkutano huo ambao ungefanyika.

“Walibaini kwamba kulikuwa na mazingira makubwa sana ya rushwa kwa wajumbe wakati wakiwa huko chini, hali kama hiyo iliyokuwa imeonekana imeonyesha kwamba uchaguzi huo umegubikwa na mambo ambayo hayawezi kutoa haki kwa wana TLP wote kwa ujumla na wajumbe kwa ujumla,” amesema Lyimo.

Hata hivyo uongozi wa chama hicho uliamua kutoa posho kwa wajumbe wote walihudhuria kwa lengo la kushiriki mkutano mkuu wa chama hicho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!