September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Vurugu CUF

Spread the love

VURUGU, kutupiana maneno na kutuhumiana imekikumba Chama cha Wananchi (CUF), wakati wa maadhimisho ya miaka 19 ya mauaji ya wananchama wake viwiwani Zanzibar. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Sintofahamu hiyo imeibuka leo tarehe 27 Januari 2020, Ofisi Kuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam, baada ya kuibuka kwa kundi linalotuhumu uongozi wa chama hicho kuendesha chama kwa majungu, fitna na mihemuko.

Baadhi ya wafuasi wa chama hicho, wameibuka huku wakibeba mabango yenye jumbe mbalimbali wakielekeza tuhuma zao kwa Prof. Ibrahim Lipumba kwamba, anaendeshwa kwa majungu y

kutoka kwa maofisa wengine wa chama hicho.

Tuhuma hizo zimeibuka ikiwa si siku tatu baada ya Abdul Kambaya, aliyekuwa Mkurugenzi wa Habari, Mawasiliano na Umma wa chama hicho kujiuzulu kwa madai ya kushindwa kuhimili kile kinachoitwa ‘majungu.’

Kongamano hilo, limefanywa kutokana na maujaji ya wafuasi wa chama hicho yaliyotokea tarehe 26 na 27 Januari 2001, visiwani Zanzibar chini ya uongozi wa Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa.

Msingi wa vurugu na kutoelewana kwa wafuasi hao ni kuwa, wanakerwa na sintofahamu inayokikumba chama hicho na mwenendo wake unaoonesha kutokuwa na afya kwa siku za baadaye.

Moja ya mabango hayo, yameandika ujumbe uliopingakujizulu kwa Kambaya, kwa maelezo hakutendewa haki kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa kwenye chama hicho.

Pamoja na hivyo, ujumbe huo unaeleza kwamba Kambaya ni miongoni mwa waathirika wa Januari 26 na 27, na kwamba kwa sasa anaonekana ‘hafai.’

Hata hivyo, walinzi wa chama hicho walifanikiwa kutuliza munkari ya wafuasi hao, ambapo walikuwa tayari wamevuruga utaratibu wa maadhimisho hao.

Kambaya alijiuzulu hivi karibuni, ambapo taarifa ya chama hicho haikueleza sababu za kujiuzulu kwake, hata hivyo mwanasiasa huyo kijana aliuambia mtandao huu kwamba;

“Anayepaswa kueleza sababu za kujiuzulu kwangu ni Prof. Lipumba. Mwambie awaeleze maana niliziandika kwenye barua yangu ya kujiuzulu.”

Visiwani Zanzibar, jana tarehe 26 Januari 2020 waliokuwa viongozi wa CUF, walifanya kongamano hilo. Viongozi hao kwa sasa ni viongozi na wafuasi wa Chama cha ACT-Wazalendo, akiwemo Maalim Seif Sharif Hamad na Babu Juma Duni Haji.

error: Content is protected !!