December 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

VPL: Yanga kutabasamu, Simba kuendeleza ubabe?

Spread the love

 

MTIFUANO wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2020/21, inaendelea leo Jumamosi tarehe 17 Aprili 2021 na kesho Jumapili, katika viwanja mbalimbali nchini humo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Leo Jumamosi, kutakuwa na michezo mitatu huku vinara wa ligi hiyo, Yanga ikiwaalisha wafanyabiashara kutoka mkoani Mara, Biashara United.

Mchezo huo utachezwa kuanzia saa 1:00 usiku, kwenye dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, huku Yanga ikiwa na shauku ya ushindi ili kurejesha furaha kwa mashabiki.

Itakuwa inashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu ya droo dhidi ya KMC kwenye mchezo uliopita huku watani zao, Simba ikishuka dimbani kesho Jumapili, Uwanja wa CCM Karambare dhidi ya Mwadui FC.

Simba ambayo ni bingwa mtetezi, inashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu ya kutoa kipigo cha 5-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Wachezaji wa Simba SC wakiwa mazoezini

Michezo mingine inayochezwa leo ni ule wa kuanzia saa 8:00 mchana Coastal Union dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mkwakwani-Tanga; saa 10:00 jioni ni vijana wa Sugar yaani Mtibwa Sugar dhidi ya Kagera Sugar.

Mpaka sasa Yanga imeshuka dimbani mara 24 ikiwa na pinti 51, Azam imecheza michezo 26 ikiwa na pointi 50 huku Simba yenye pointi 49, imeshuka dimbani mara 21 huku Biashara United ikiwa nafasi ya nne na pointi zake 40, kati ya michezo 25.

Mwadui inashika mkia, ikiwa na pointi 16, baada ya kucheza michezo 25 huku Mbeya City ikiwa ya pili kutoka mwisho ikiwa na pointi 21 kati ya michezo 25 iliyocheza.

error: Content is protected !!