December 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Vodacom yazindua promosheni mpya ya “Amsha Ndoto, Amsha Shangwe”

Spread the love

 

VODACOM Tanzania PLC imezindua promosheni ya wiki nane katika msimu huu wa siku kuu iitwayo “Amsha Ndoto, Amsha Shangwe” itakayowapa wateja wake fursa ya kujishindia zawadi mbali mbali ikiwemo pesa taslimu hadi Sh 10 milioni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akitangaza promosheni hiyo leo Ijumaa tarehe 18 Novemba, 2022, Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania plc, Philip Besiimire amesema kutakuwa na mshindi mmoja wa Tsh 10 kila wiki na washindi watano kila siku wa Tsh 1,000,000. Vile vile wateja watakuwa na nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo simu janja, TV janja, mifumo ya 5G, bima ya VODA BIMA na usafiri wa bure kupitia Paisha.

Amesema wateja wa Vodacom wanaweza kushiriki kwenye promosheni hiyo na kupata nafasi ya kujjishindia zawadi mbalimbali kwa kufanya manunuzi na miamala kupita M-Pesa kwa kipindi hiki cha promosheni, pamoja na kutumia huduma za usafiri wa Paisha.

“Miamala yote itakayofanyika kupitia M-Pesa kwa kipindi hiki cha promosheni itaingia kwenye droo na kumpa mteja nafasi ya kushinda,” amesema Besiimire.

Ameongeza kuwa Vodacom imekuwa na utamaduni wa kuwatunuku wateja msimu wa sikukuu kuonesha jinsi Vodacom inathamini mchango wao.

“Msimu wa siku kuu ni muhimu na unahamasa kwetu sote. Tunapata fursa ya kupumzika na kuwa na wapendwa wetu vile vile kutafakari mafanikio yetu ya mwaka wakati tunaweka malengo ya mwaka ujao.

Kipindi hiki kawaida tuna utaratibu wa kutembelea familia zetu na kuwanunulia zawadi, na sisi kama Vodacom familia yetu ni wateja wetu na ndio sababu ndani ya miaka michache iliyopita tulianzisha utaratibu wa kuwapa zawadi wateja wetu ili kufanya msimu huu wa sikukuu uwe wa furaha zaidi kwao,”amesema Bisiimire.

Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania plc, Philip Besiimire

Amesema Vodacom ina matumaini ya kusaidia kufanikisha ndoto za wateja wake hasa kipindi hiki cha msimu wa sikukuu na kutoa wito kwa wateja wa Vodacom kutumia M-Pesa kufanya miamala na kujiongezea nafasi za kushinda zawadi kubwa.

“Inawezekana ulitaka kumiliki gari, kuanzisha biashara, kulipa ada ya shule, kumalizia ujenzi wa nyumba au kwenda kupumzika, sisi Vodacom tungependa kukusaidia kufanikisha ndoto yako.

Tunaamini zawadi tutayokupa utasambaa furaha kwa wateja wetu. Masta Shangwe wetu atatembelea nnchi nzima kusambaa upendo na furaha,” amesema.

Promosheni hiyo inapatikana kwa wateja wote wa Vodacom ambapo mteja atasema kitu anachotaka kushinda kupitia M-Pesa App au USSD kwa kupiga *150*00# na kuwa kwenye nafasi ya kujishindia mamilioni na zawadi nyingine.

error: Content is protected !!