July 31, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Vodacom yaja na mfumo mpya ununuzi magazeti

Spread the love

KAMPUNI ya Simu za Mkononi (Vodacom) leo imezindua mfumo mpya wa kununua magazeti na majarida kupitia simu za mkononi za kisasa (smartphone) kwa kupakua ‘application’ inayoitwa m-paper, anaandika Faki Sisi.

Vodacom imezindua mfumo huo kwa kushirikiana na Kampuni ya Smart Codes inayomiliki m-paper na kwamba, mfumo huo utamuwezeza mteja kupata magazeti na majarida mapema kuliko ilivyo sasa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo leo Jijini Dar es Salaam, Rosalynn Mwaria, Ofisa Uhusiano wa Vodacom amsema kuwa, wateja wa mtandao wa Vodacom wataweza kupakuwa magazeti na majarida hayo wakati wowote.

Amesema kuwa, kupitia mfumo huo mpya mteja atanunua gazeti kwa nusu bei ya sasa (kama linauzwa 500, kwenye m-paper atanunua kwa Sh. 250).

Mwaria amesema kwamba, mteja anaweza kununua magazeti hayo likiwemo MwanaHALISI na MSETO kwa kutumia salio lake la m-pesa au salio la muda wa hewani wa maongezi na kuwa, walio nje ya nchi wanaweza kununua kwa kutumia kadi zao za benki za Amercan Express, Visa card.

Edwin Bruno, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Smart Codes amesema kuwa, wameamua kushirikiana na Vodacom kuleta huduma hii ili kumrahisishia mteja.

“Hivi sasa tunaishi katika Ulimwengu wa sayansi na teknolojia imekuwa ikibadilika siku hadi siku ambapo hivi sasa mifumo inayotumika ni ya kidigitali,” amesema.

 

error: Content is protected !!