Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Vodacom wamponza Mkurugenzi TCRA
Habari za Siasa

Vodacom wamponza Mkurugenzi TCRA

Mhandisi Izack Kamwelwe, Waziri wa Uchukuzi, Usafirishaji na Mawasiliano. Picha ndogo, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kulaba
Spread the love

MHANDISI Izack Kamwelwe, Waziri wa Uchukuzi, Usafirishaji na Mawasiliano amempa siku 30 Mkurugenzi wa Mawasiliano Tanzania  (TCRA) kuzungumza na Kampuni ya Mtandao wa simu ya  Vodacom Tanzania kutatua kero ya wizi wa fedha unaofanya kupitia mtandao huo. Anaripoti Khalifa Abdallah … (endelea).

Kamwelwe amesema hayo leo akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za TCRA wakati kampuni hiyo ikipatiwa leseni ya Masafa marefu ya 700MHz itakayowezesha kutanua wigo wa mawasiliano kwa kampuni hiyo.

“Nendeni mkakae mfikirie kabla sijatoa maelekezo ili mtu akiniibia kwenye simu yangu kwenye yangu ya Vodacom kampuni iwajibike kurudisha, mna wafanyakazi ambao wapo nje ya mfumo, lakini lazima mliwaajiri na mkawafukuza hao ndiyo wanaotuibia,” amesema Kamwelwe.

Katika hatua nyingine Kamwelwe amesema kuwa daraja la kisasa la Salander linalotarajiwa kujengwa na Tanzania katika barabara inayotokea Coco Beach hadi kutokea Agha Khan ni daraja la kwanza kutokea Tanzania.

Daraja hilo lililogharimu Dola za Marekani 126 milioni linatarajiwa kuwa ni urefu wa Km 1 na Mita 30.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

error: Content is protected !!