Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Vodacom waadhimisha siku ya Wanawake kwa jukwaa la Women’s Network Forum
Habari Mchanganyiko

Vodacom waadhimisha siku ya Wanawake kwa jukwaa la Women’s Network Forum

Spread the love

Mkurugenzi wa Fedha Vodacom Tanzania Plc, Hilda Bujiku (mwenye kipaza sauti) akizungumza wakati wa jukwaa la Women’s Network Forum lililoandaliwa na kampuni hiyo kujadili nafasi iliyonayo katika kuleta usawa kwenye huduma za kidigitali Tanzania ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa kila ifikapo Machi 8 ya kila mwaka.

Wakimsikiliza ni jopo la majaji kutoka Vodacom Tanzania Plc walioshiriki jukwaa hilo la majadiliano kulia kwake ni Athumani Mlinga, Mkurugenzi wa Teknolojia ya Mawasiliano na kwenda kushoto kwake ni Mcberthana Wilfred, Meneja wa Usalama wa Mtandaoni na Teknolojia ya Mawasiliano, Niamini Yonazi, Mtengeneza Programu, na Aileen Meena ambaye alikuwa ni mwendesha mjadala.

Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Vodacom Tanzania Plc, Vivienne Penessis akizungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati wa jukwaa la Women’s Network Forum lililoandaliwa na kampuni hiyo kujadili nafasi iliyonayo katika kuleta usawa kwenye huduma za kidigitali Tanzania ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa kila ifikapo Machi 8 ya kila mwaka. Kauli mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka huu ni ‘Ubunifu na Teknolojia kwa usawa wa kijinsia’.

Niamini Yonazi, Mtengeneza Programu wa Vodacom Tanzania Plc akizungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo (hawapo pichani) wakati wa jukwaa la Women’s Network Forum lililoandaliwa na kampuni hiyo kujadili nafasi iliyonayo katika kuleta usawa kwenye huduma za kidigitali Tanzania ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa kila ifikapo Machi 8 ya kila mwaka. Kulia ni Meneja wa Usalama wa Mtandaoni na Teknolojia ya Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Plc, Mcberthana Wilfred, na kushoto ni Aileen Meena ambaye alikuwa ni mwendesha mjadala.

Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc wakifuatilia kwa makini wazungumzaji wa jukwaa la Women’s Network Forum (hawapo pichani) lililoandaliwa na kampuni hiyo kujadili nafasi iliyonayo katika kuleta usawa kwenye huduma za kidigitali Tanzania ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa kila ifikapo Machi 8 ya kila mwaka. Kauli mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka huu ni ‘Ubunifu na Teknolojia kwa usawa wa kijinsia’.

Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc wakiwa kwenye picha ya pamoja ikiwa ni ishara ya kukumbatia usawa wa kijinsia kwenye ubunifu na teknolojia kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa kila ifikapo Machi 8 ya kila mwaka. Kusherehekea siku hiyo jukwaa la kampuni hiyo la Women’s Network Forum lilikutana na kujadili mada zinazohusiana na ubinifu na teknolojia katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!