January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Vodacom, TFF wafunga ndoa udhamini VPL

Spread the love

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF) limesaini mkataba mpya wa miaka mitatu wa udhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) wenye thamani ya Sh. 6.6 bilioni na kampuni ya simu ya Vodacom, halfa hiyo imefanyika leo katika ofisi za makao makuu ya kampuni hiyo eneo la Mlimani City jijini Dar es salaam.

Akiongea wakati wa kusaini mktaba huo mpya, Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom, Kelvin Twissa, amesema kampuni yao inafurahia kuendelea kuwa sehemu ya udhamini ya ligi kuu nchini, mafanikio ya timu bora na kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa inatokana na kuwa na ligi bora ambayo inadhaminiwa na Vodacom.

Naye Rais wa TFF, Jamal Malinzi amewashukuru kampuni ya Vodacom kwa kukubali kuendelea kuidhamini ligi kuu kwa kipindi kingine cha miaka mitatu na kuongeza sehemu ya udhamini wao kwa asilimia 40%.

Mkataba huo mpya wa udhamini kwa kipindi cha miaka mitatu, umeboreshwa na kuwa na ongezeko la asilimia 40% kutoka katika mkataba wa awali uliomalizika.

Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 12, 2015.

error: Content is protected !!