KAMPUNI ya ya Mawasiliano ya simu za mikononi ya Vodacom Tanzania pamoja na Smart Lab imezindua mpango maalam wa kuwawezesha wajasiriamali wadogo nchini. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Mpango huo ulipewa jina la “Vodacom Digital Accelerator” umezinduliwa leo tarehe 25 Aprili 2022 jijini Dar es Salaam ambapo Mkurugenzi wa Digital na Huduma za Ziada wa Vodacom, Nguvu Kamando amesema kuwa mpango huo utagharimu kiasi cha shilingi 500 Milioni na kwamba lengo ni kuwapa nguvu na uzoefu wajasiriamali.
“Kwa mara nyingine Vodacom inajivunia kuwa sehemu ya programu hii tukiendelea kutekeleza ari yetu ya ‘pamoja tunaweza’, kupitia progamu hii tuna nia ya kuwawezesha na kuwapa uzoefu wajasiriamali nchini,” amesema Kamando.
Ameongeza kuwa, “uvumbuzi na ujarisiamali ndio mzizi mkuu katika kuhakikisha zana yetu ya kuipeleka Tanzania katika ulimwengu wa kidijitali na tumepata uzoefu mkubwa kufanya kazi kushirikiana na Smart Lab ambao wamejikita kutoa mafunzo na kuwaongoza wajasiriamali wanaoshiriki.
Amesema kuwa Mafanikio ya programu hii ni kuona maendeleo yanayofanywa na kampuni chipukizi zinazoshiriki ikiwa ni pamoja na kukua kwa mtaji kutoka kwa wawekezaji, kumalizika kwa uundwaji wa bidhaa na kukua kwa watendaji wa kampuni.
Msimu wa kwanza wa programu ya “Vodacom Digital Accelerator” ulizinduliwa mwaka 2019 na kupokea maombi 500 kutoka mikoa 18 nchini ambapo kufikia mwisho wa program, kampuni chipukizi nne ziliibuka washindi.

Kampuni zilizoshinda ni pamoja na Smartclass inayojihusisha na masuala ya elimu, Hashtag Pools inayoshughulika na masuala ya biashara ya kimtandao na kampuni mbili za masuala ya afya ambazo ni Nisiima eDispensary na MyHI.
Programu ya mwaka huu inategemewa kuwa kubwa na bora zaidi na itaendelea kujikita kufanya kazi na kampuni chipukizi zinazojihusisha na masuala ya mawasiliano, habari, afya, elimu, kilimo, utalii na biashara ya kimtandao.
Utelekezaji wa programu hii utashirikisha wadau na washirika mbalimbali. Baada ya kupokea maombi, kampuni zitakazochaguliwa zitatakiwa kuwasilisha maendeleo yake kwa wawekezaji baada ya miezi mitatu ambapo watakaovuka hatua hii watapata ushirikiano kutoka Vodacom, Smart Lab na washirika wengine kwa muda wa miezi sita.
Mkurugenzi Mtendaji wa Smart Africa Group (SAG), Edwin Bruno ambaye pia ni mshirika wa Smart Lab, amesema, “tunafurahi kuwa sehemu ya ‘Vodacom Accelerrator’ na kwa pamoja tunatarajia kutengeneza fursa kwa vijana waliojikita kwenye teknonojia ili kukuza kampuni na kazi zao na kuonyesha kuwa vijana wa kitanzania wanaweza kushindana kwenye level ya kimataifa kwenye masuala ya ujasiriamali uliojikikita kwenye ya teknolojia.
Ameongeza kuwa, “shughuli za kivumbuzi nchini zimepiga hatua kubwa miaka michache iliyopita na Smart Lab pamoja na Vodacom Tanzania tumeongoza njia hasa hasa kwenye uvumbuzi kupitia makampuni ya biashara na kuonyesha vijana kuwa inawezekana kujenga kampuni zikafanikiwa nchini, kama ambavyo Smart Africa Group na Vodacom zilijengwa nchini Tanzania
Leave a comment