Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Vodacom kutangaza washindi wa programu ya Vodacom Digital Accelerator
Habari Mchanganyiko

Vodacom kutangaza washindi wa programu ya Vodacom Digital Accelerator

Spread the love

 

KAMPUNI ya Vodacom Tanzania PLC inatarajia kutangaza kampuni bunifu chipukizi tatu zilizoibuka na ushindi wa msimu wa pili wa programu ya Vodacom Digital Accelerator iliyofanyika kwa kushirikiana na Smart Lab. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).  

Washindi hao watapatikana baada ya kuwasilisha na kuonyesha shughuli wanazozifanya kwa jopo la majaji waliobobea kwenye maeneo ya teknolojia, ujasiriamali, uwekezaji na sheria, ambapo uwasilishaji wa maonyesho hayo unatarajiwa kufanyika tarehe 3 Machi, 2023, katika hoteli ya Hyatt Regency ya jijini Dar es Salaam.

Msimu huo wa pili wa Vodacom Digital Accelerator ulianza mwezi Aprili, 2022 kwa kupokea maombi kutoka kwa kampuni zote bunifu chipukizi za kiteknolojia za Kitanzania zenye mustakabali wa kukua.

Kampuni 12 zilichaguliwa kujiunga na programu hii na kuingia kwenye hatua ya kujengewa uwezo ambapo zilipatiwa msaada wa ziada kwenye kukuza mikakati yao ya kimasoko, eneo la kiufundi, na kuwaunganisha kwa washirika na wawekezaji.

Kampuni hizo bunifu chipukizi zinatoka kwenye sekta tofauti ambazo ni pamoja na huduma za kiteknolojia za kifedha, afya, biashara za mtandaoni, elimu, kilimo, na usalama wa mtandaoni.

“Tumefurahi kufikia hatua hii ya programu yetu ya Vodacom Digital Accelerator ambapo tumefanikiwa kuona namna ilivyosaidia kukuza ubunifu kwa kampuni chipukizi za Kitanzania, uwasilishaji tutakaojionea kwenye maonyesho ndio utasaidia kuwatambua washindi watatu, ambao watazawadiwa zaidi ya Sh. 200 milioni.

“Ningependa kutoa wito kwa wadau kwenye sekta ya ubunifu na teknolojia kujisajili kwa njia ya mtandaoni ili kushiriki wakiwa popote walipo siku ya kesho,” alisema Nguvu Kamando, Mkurugenzi wa Huduma za Kidigitali, Vodacom Tanzania PLC.

Kamando alisema watu wote wanakaribishwa kujiunga nasi au kusikiliza uwasilishaji wa maonyesho hayo na kuweza kuzipigia kura kampuni bunifu chipukizi bora kupitia kiambatanisho (link) ambacho kitapatikana kwenye kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya kampuni.

Kampuni bunifu chipukizi ambazo zimefikia hatua ya fainali ni pamoja na Shule Yetu Innovations, Smart Darasa, Lango Academy, na Vijana Tech, kwa upande wa huduma za elimu za kiteknolojia. Hack it Consultancy inawakilisha eneo la huduma za usalama wa mtandaoni. Seto, Twenzao, Get Value, na Spidi Africa zipo chini ya biashara za mtandaoni. Nyinginezo ni Medpack ikiwakilisha huduma za afya za kiteknolojia, zikiwemo na, Bizy Tech Pamoja na Bizzy Pay ambazo zenyewe zipo upande wa huduma za kifedha za kiteknolojia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!