VJOSA Osmani-Sadriu (38), ameapishwa kuwa Rais wa Kosovo, na kaundika historia ya kuwa mwanamke wa kwanza mwenye umri mdogo duniani kushika wadhifa huo. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).
Leo tarehe 7 Aprili 2021, Bunge la Kosovo limemuapishwa Sadriu kuwa rais wa taifa hilo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Awali, Sadriu alichukua madaraka Ikulu muda mchache baada ya aliyekuwa rais wa taifa hilo, Hashim Thaci kujiuzulu kutokana na shinikizo lililobebwa na machafuko na uvunjifu wa haki za binadamu nchini humo.
Hatua ya Bunge la Kosovo lenye wabunge 128, lilimchagua Sadriu kwa kura 71 dhidi ya kura 11 zilizomkataa, kura 38 zilitajwa kuharibika ambapo wabunge wanane hawakupiga kura.
Hata hivyo, wabunge wapinzani walipinga matokeo ya kura hizo wakudai, ulitawaliwa na visa.
Kukimbia ofisi kwa aliyekuwa rais wa taifa hilo – Thaci, kulitoa nafasi kwa Sadriu kutawala Ikulu kuanzia Desemba 2020 mpaka mwishoni mwa Machi 2021, ambapo taratibu za kumpata rais wa miaka mitano ijayo zilipoanza.
Thaci amefikishwa katika Mahakama ya Uhalifu wa Kivita (The Hague), kujibu tuhuma zake kuhusu uhalifu na uvunjifu wa haki za binadamu kwa raia wa Kosovo.
Thaci alianza kuongoza taifa hilo miaka ya 1990 akitoa msituni ambapo aliendesha mpambano ya Kosovo kujiondoa katika utawala wa Serbia.
Uhuru wa Kosovo ulipatikana mwaka 2008 ambapo ulipongezwa na mataifa zaidi ya 100 duniani, hata hivyo Serbia, Urusi na China zilijitenga na pongezi hizo.
Kabla ya kushika wadhifa huo, Sadriu alitoa mchango mkubwa wa mahusiano kati ya taifa hilo na mataifa mengine duniani, lakini aliwahi kuwa mmoja wa viongozi wa juu wa vikosi vya jeshi la nchi hilo.
Hataree hiyo