Wednesday , 17 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Vituo chanjo ya Corona vyaongezwa, Msigwa awapa neno wasiochanjwa
AfyaHabari Mchanganyiko

Vituo chanjo ya Corona vyaongezwa, Msigwa awapa neno wasiochanjwa

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania imeongeza vituo vya utoaji huduma ya chanjo ya ugonjwa wa Corona (UVIKO-19), kutoka 550 hadi 6,784 nchi nzima. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumapili, tarehe 19 Septemba 2021 na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, akizungumza na wanahabari jijini Dodoma.

“Zoezi linalofanyika sasa tulikuwa na vituo 550 tumeongeza kwenda vituo 6,784. Yaani vituo vyote vya Tanzania vinavyotoa chanjo mbalimbali, sasa vinapewa chanjo ya uviko 19- Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa.

Akitaja takwimu za watu waliopata chanjo tangu zoezi hilo lizunduliwe na Rais Samia Suluhu Hassan, mwishoni mwa Agosti 2021, Msigwa amesema watu 360,000 wamepata chanjo hiyo.

“Katika zile chanjo 1,540,400 za UVIKO-19, chanjo takribani  360,000 tayari Watanzania wameshapewa chanjo,” amesema Msigwa.

Gerson Msigwa, Msemaji wa Serikali

Msigwa amesema, Serikali iko katika mpango wa pili wa kuhimiza wananchi kupata chanjo ya UVIKO-19, ambapo watalaam wanaotoa huduma hiyo wanawafuata wananchi katika maeneo yao, hasa vijijini.

Msigwa amesema, Serikali imeanza mpango huo ili chanjo hizo ziwafikie wananchi wengine.

“Kazi inayofanywa na Serikali kwenye mpango wa pili wa kuhimiza chanjo, wataalamu wanatoka kwenye vituo wanakwenda kuwafuata wananchi vijijini, Watanzania wote wapate fursa ya kupata chanjo ya UVIKO-19 kule waliko, kupitia huduma ya mkoba,” amesema Msigwa.

Aidha, Msigwa amewaomba Watanzania wasiopata huduma hiyo, wakachanjwe ili kukwepa athari za janga hilo linaloitikisa dunia.

“Sitaki kuwatisha, lakini ningependa kuwaambia Watanzania, takwimu za wataalamu wa afya watazitoa karibuni. Lakini kwa sehemu kubwa ya watu waliolazwa kutokana na UVIKO-19, ambao wapo kwenye hali mbaya ni wale ambao hawajachanjwa,” amesema Msigwa na kuongeza:

“Wale waliochanjwa ukipatwa na UVIKO-19, unapewa matibabu unatoka unaenda nyumbani unaendelea na kazi zako, wasio chanjwa hoi taaban wamewekwa mashine. Wanapumua kwa msaada wa mashine na wanaokufa kwa sehemu kubwa ni wale wasiochanjwa.”

2 Comments

  • Taarifa kuhusu chanjo na Uviko ilipaswa itolewe na waziri wa afya au na katibu mkuu wake badala ya Msigwa. Haya ni mambo ya kitaalamu sawa na mitihani ya shule. Msigwa hahusiki

    Pili, ni wananchi wachache wamechanjwa. Tuwe na mkakati. Viongozi wote wa mkoa na wilaya na hata vijiji waoneshe mfano kwa kuchanjwa hadharani kama alivyofanya Rais. Viongozi wa kidini na vyama vya siasa nao wahusishwe. Haitoshi kuhubiri tu faida ya kuchanjwa. Tuoneshe mfano

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Sekta binafsi yasifu utekelezaji wa Mkumbi

Spread the loveSERIKAL imepongezwa kwa utekelezaji wa mapendekezo ya sekta binafsi kupitia...

Habari Mchanganyiko

Kamati ya bunge yapigia chapuo kilimo ikolojia

Spread the loveSERIKALI kupitia Wizara ya Kilimo imeshauriwa kushirikiana na wadau wa...

Habari Mchanganyiko

Serikali yapata hasara 113 milioni hospitali kuwapa misamaha wagonjwa wasiostahili

Spread the loveSERIKALI imepata hasara ya kiasi cha Sh. 111.76 milioni, baada...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

error: Content is protected !!