June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Viti Maalum waibana serikali

Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima

Spread the love

MBUNGE wa Viti Maalum (CUF), Amina Abdallah Amour, ameitaka kueleza umma, ni lini itatenga bajeti ya asilimia 30 kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambayo imekuwa ikikwama kila mwaka. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Amour aliyasema hayo jana wakati akiuliza swali la nyongeza jana bungeni mjini Dodoma. Awali alitaka kufahamu, mkakati wa serikali wa kuondokana na bajeti tegemezi.

Mbunge huyo pia alitaka kujua ni kwa nini wafadhali wanakataa kutekeleza ahadi zao hivyo kuharibu utaratibu wa bajeti.

Akijibu maswali hayo Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima alisema, mchakato wa bajeti ya maendeleo kufikia asilimia 30 hadi 40 kwa kila bajeti ni jambo gumu kutekelezeka kutokana na ukata unaoikabili serikali.

Alisema serikali imekuwa na mipango mingi ya kuhakikisha inafikia katika kipato ambacho kitaondoa utegemezi. Hata hivyo, alisema mchakato huo hauwezi kutekelezwa kwa njia ya kufumba na kufumbua.

Alisema, “Nakiri kuwa bado uwezo wa serikali kutenga asilimia 30 hadi 40 ya bajeti ya maendeleo hatujaufikia; lakini mipango yetu ni kupunguza utegemezi na mwaka huu utegemezi umefikia asilimia 10.”

Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mbozi Magharibi (Chadema), David Silinde aliyetaka kujua serikali mikakati ya serikali ya kuongeza ukusanyaji wa mapato, Malima alisema suala la kuongeza mapato ni muhimu likapiganiwa na kila mbunge.

“Serikali itaongeza juhudi za ukusanyaji wa mapato, ila tutaendelea kukopa ili kutekeleza miradi mbalimbali,” alieleza.

error: Content is protected !!