Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Vitendo vya wanaume kutekeleza watoto vyatikisa Bunge, latoa maagizo
Habari za Siasa

Vitendo vya wanaume kutekeleza watoto vyatikisa Bunge, latoa maagizo

Dk. Tulia Ackson, Spika wa Bunge la Tanzania
Spread the love

 

VITENDO vya baadhi ya wanaume kutelekeza watoto kwa kutogharamia matunzo yao, vimezua mjadala bungeni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Mjadala huo umeibuka leo Ijumaa tarehe 21 Mei 2021, baada ya Mbunge Viti Maalum (CCM), Neema Kichiki Lugangira, kuhoji mikakati ya Serikali katika kuwasaidia wanawake wanaobebeshwa mzigo wa kugharamia watoto wao, baada ya wenza wao kuwatelekeza.

“Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwakomboa Wanawake wanaobebeshwa mzigo mkubwa wa kugharamia matunzo ya Watoto bila msaada wa Baba?” amesema Lugangira.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mwanaidi Khamis, alimjibu kwa kusema, Serikali iliandaa Sheria ya Mtoto Namba 21 (2009), ili kutoa maelekezo juu ya wajibu wa wazazi katika kuwahudumia watoto, ili kukabiliana na vitendo hivyo.

“Katika kuwakomboa wanawake hawa wanaobebeshwa mimba na kuachwa bila matunzo, Serikali imeandaa Sheria ambayo pamoja na masuala mengine inatoa maelezo kuhusu matunzo kwa mtoto kutoka kwa wazazi wote wawili,” amesema Mwanaidi.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mwanaidi Khamis

Naibu Waziri huyo wa Afya amesema “sheria hii kupitia kifungu cha 44 (a – e) na Kifungu cha 45(1), imetoa maelezo endapo wazazi wa mtoto kama hawaishi pamoja na kama mtoto atakuwa anaishi na mzazi wake wa kike yaani mama, basi mzazi wa kiume atawajibika katika kugharamia malezi, kulingana na kipato alichonacho na mazingira anayoishi mtoto husika.”

Kufuatia majibu hayo, Lugangira alisema sheria hiyo imepitwa na wakati na kuitaka Serikali iifanyie marekebisho ili iendane na wakati.

“Sheria zilizopo bado kuna changamoto kubwa katika eneo hilo, kwa msingi huo naomba kuuliza, serikali haioni haja kurekebisha sheria ziliopo ili gharama za matunzo ya watoto iendane na hali uchumi wa sasa,” amesema Luganriga.

Mbali na Lugangira, Mbunge Viti Maalum, asiye na chama bungeni, Hawa Mwaifunga, aliishauri Serikali ilete bungeni mabadiliko ya Sheria ya Ustawi wa Jamii, ili iendane na mazingira ya sasa.

Naye Mbunge wa Mbulu Mjini (CCM), Zacharia Isaay alihoji “Pamoja na majibu mazuri ya Serikali kupitia wizara ya afya, tatizo la waliotekelezwa limekuwa kubwa. Haioni ni wakati muafaka kutazama upya sheria ili kuzuia uwepo wa watoto wa mitaani kwa ajili ya wanaotelekeza watoto.”

Akijibu mjadala huo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima, amesema Serikali itafanyia kazi ushauri huo.

“Ni kweli Serikali inatambua tatizo hili ni kubwa na tunakiri kuna haja ya kufanya kitu cha ziada hapa. Kuelekea maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika, tunapoadhimisha siku hiyo tutaongelea suala hilo,”
Kuhusu Maafisa Ustawi wa Jamii kutengewa bajeti za kuhudumia watoto wa mtaani, Dk. Gwajima amesema Serikali itafanya tathimini kubaini ukubwa wa changamoto hiyo.

Na kwamba katika bajeti ijayo (2021/2022), itaanzisha utaratibu wa kwuawezesha maafisa ustawi wa jamii, kwa ajili ya kushughulikia suala hilo.

“Ni kweli Serikali inatambua hatujawekeza eneo hilo kuwezesha maafisa ustawi wa jamii kushughulikia watoto wa mitaani, tutafanya tathimini tuone kipindi kijacho cha bajeti kuanzisha namna ya kuwawezesha maafisa hao,” amesema Dk. Gwajima.

Baada ya mjadala huo kumalizika, Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson alitoa agizo kwa Chama cha Wabunge Wanawanake, kijikite katika kutoa elimu kwa wanawake, juu ya uzazi wa mpango ili wazae watoto wanaoweza kuwahudumia, bila ya msaada wa wanaume.

“Waheshimiwa wabunge wanawake chini ya Mwenyekiti wetu Shari Raymond, ni vizuri na sisi tuchukue hatua kwenye maeneo hayo. Lazima wanawake tuondokane na hii dhana ya mtu kubebeshwa mimba,” amesema Dk. Tulia.

Naibu Spika huyo wa Bunge amesema “ sababu yeye ndio anabeba mimba, lazima tuzungumze na wanawake watumie uwezo wao aidha ya ushaiwishi au wafanye hayo mambo ya kubeba mimba kwa wataoto wanaoweza kuwalea hata kama huyo mwanaume hayupo.”
Dk. Tulia ameshauri wanawake wapewe elimu juu ya maamuzi sahihi ya kuepuka migogoro ya kifamilia.

“Ni kazi yetu wabunge wanawake tuweke msingi mzuri sababu watoto wetu wa kike hawataweza kufikia ngazi kubwa za uongozi. Hatuwezi kupata viongozi wanawake kama tunafikiria watoto wa mitaani sababu wanaume wanakimbia. Tuwafundishe wanawake wetu wafanye maamuzi sahihi,” amesema Dk. Tulia..

1 Comment

  • Ustawi wa jamii ukishirikiana na mamlaka husika na sheria mwongozo, waanzishe kitu kinaitwa ‘child support’ ambapo mzazi aliyemtelekeza mtoto analipa kiasi cha matunzo ya mtoto kulingana na kiwango cha mapato yake, na gharama hizo zikitumwa moja kwa moja kwa mlezi wa mtoto huyo. kushindwa kufanya hivyo liwe kosa la kisheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo aungana na wananchi ujenzi maabara za sekondari

Spread the loveMBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, kwa kushirikiana na...

Habari za Siasa

CCM apiga marufuku wazazi kuwatumia watoto wa kike kwenye mambo ya kimila

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

Ofisi za mabalozi wa mashina zitumike kuwale vijana kimaadili – Chongolo

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameagiza...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

error: Content is protected !!