Wednesday , 27 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Vitambulisho vya ujasiriamali ni bomu-Chadema
Habari za Siasa

Vitambulisho vya ujasiriamali ni bomu-Chadema

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimelalamikia uanzishwaji wa mradi wa serikali wa ugawaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo na kwamba, ni bomu linalosubiriwa kulipuka. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 22 Februari 2019 na Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Chadema Zanzibar wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam.

Mwalim amesema kuwa, mradi huo utakuwa bomu kama serikali haitokuwa sikivu kwa kusikiliza ushauri na kufanya tathimini upya pamoja na kushirikisha ipasavyo wahusika.

“Mradi huu wa vitambulisho ni bomu lingine, lisipoangaliwa kwa ufasaha likatekelezwa kwa hekima na busara badala ya mabavu ni bomu linalosubiriwa kulipuka. Hili ni bomu linasuhbiri kulipuka kama serikali haitatokwua sikivu ikajirudi ikafanya tathimni upya na kupanga progamu hii kuwa shirikishi na watu kushirikishwa,” amesema Mwalimu.

Aidha, Mwalimu amehoji utaratibu uliowekwa wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya  kukusanya fedha kutoka kwa wajasiriamali hao, akisema kuwa, fedha hizo ili ziwe salama zinatakiwa kukusanywa na Malamka ya Mapato Tanzania (TRA).

“Kuna taarifa tunaaMbiwa mradi huo unalenga kukusanya zaidi ya Sh. 20 bilioni unasiammiwa na wakuu wa mikoa na wilaya, kodi za nchii tangu lini zinasimamiwa na wakuu wa wilaya na mikoa badala ya mamlaka ya mapato au halmashauri husika, hao wakuu wa wilaya na mikoa wakizichukua wanazipeleka wapi, risiti hizi zina nguvu kisheria kwa kiasi gani, ndio maana tunasema hili ni bomu linalosubiri kulipuka,” amesema na kuongeza Mwalimu.

“Fundi saa, fundi saloni inasemekana wote watahusika na mradi huo wa kitambulisho, hizi bilioni 20 zikishakusanywa zinakwenda wapi.”

Katika hatua nyingine, Mwalimu amesema Chadema haikubaliano na hatua ya Jeshi la Polisi mkoani Mbeya kumhoji Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kufuatia kauli yake aliyoitoa kuhusu mradi huo katika mkutano wake wa hadhara na wakazi wa jimbo lake.

“Tunasema kama chama mradi wa vitambulisho ni bomu lialosubiri kulipa wakati wowote, jeshi la polisi wasifikiri ni Sugu, Msigwa,  Heche,  Bulaya,  Mdee au ni wabunge, malalamiko ni makubwa watu wanakosa pa kupumulia ni bomu linalotarajia kulipuka.Tunasisitiza kwamba hatukubaliani na uonevu unaofanywa kwa Sugu,” amesema Mwalimu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!